KMC yaimarisha benchi la Ufundi

Friday February 28 2020

 

By Saddam Sadick, Mwanza

KLABU Klya KMC imemuongeza kikosini, Habibu Kondo kuwa Kocha Msaidizi ili kuweza kuisaidia timu hiyo kubaki kwenye  Ligi Kuu msimu ujao.
Timu hiyo ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni msimu wake wa pili kushiriki Ligi Kuu, imekuwa na matokeo yasiyoridhisha kwani katika michezo 24 iliyocheza, imekusanya pointi 21 na kukaa nafasi ya 19.
Kama haitoshi, timu hiyo ilikubali kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Kagera Sugar, kwa mabao 2-0 kwa njia ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika sare ya bao 1-1, mchezo uliopigwa juzi Jumatano mjini Bukoba.
Kondo amethibitisha kumalizana na mabosi hao, ambapo makubaliano yao ni kuitumikia kwa kipindi hiki kilichobaki kumaliza msimu, huku malengo ikiwa ni kuibakiza timu Ligi Kuu.
"Nashukuru kikao kimeenda vizuri kwa kukubaliana kuinoa timu kwa msimu huu uliobaki kisha mengine yataendelea huko mbeleni, nitakuwa chini ya Kocha Mkuu HarunaHererimana" amesema Kondo

Advertisement