Jezi za mastaa wa kigeni Yanga zatawala Taifa

Sunday August 4 2019

 

By YOHANA CHALLE

ASILIMIA kubwa ya mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Taifa kuushuhudia mchezo wa kirafiki baina ya wenyeji Yanga na Kariobangi Sharks ya Kenya wamevaa jezi za wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.
Majina ya wachezaji Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Mustapha Suleiman na Sadney Ukhrob huku majina ya wachezaji wa ndani jezi ya Kelvin Yondan na Abdulaziz Makame nazo zikitamba jukwaani.
Kundi kubwa la mashabiki hao walikuwa wamevaa jezi ambayo itatumika kwa michezo mbalimbali ya Ligi  Kuu na ile ya Kimataifa inapokuwa nyumbani ambayo imetawaliwa sehemu kubwa na rangi ya njano.
Mashabiki hao walikuwa wakifurahi kwa kupeperusha vipeperushi maalumu vilivyoandikwa 'Wiki ya Mwananchi' huku wakicheza wimbo wa timu hiyo.

Advertisement