Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Farid amfunda Tshabalala

WINGA wa Yanga, Farid Mussa ameona kitu kwa beki wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwamba akiamua kujifunza kufunga, atakuwa habari nyingine katika Ligi Kuu Bara (VPL).

Yanga imemsajili Farid akitokea Tenerife B ya Hispania ambako amecheza miaka mitano, tangu ajiunge nao 2016, alisema Tshabalala ni beki hatari anayeweza kufanya vitu vingi ndani ya dakika 90.

“Tunaocheza naye ndani ndio tunajua hatari ya Tshabalala, ambaye ni fundi wa pasi zake, sema tu simuoni kufunga hata akiwa kwenye nafasi hiyo, kama ataamua kujifunza kufunga basi atafanya mambo makubwa zaidi ya haya.

“Mfano Kapombe (Shomary) ambavyo soka lake lina mvuto ni kwa sababu ya namna ambavyo anaweza akaibia na majukumu ya watu wengine au mnyumbulikaji, anakaba, anatoa pasi na kufunga vitu ambavyo havifanywi na kila mtu.

“Kila mtu ni mchezaji ila ubora wa mtu ama kujitofautisha na wengine, lazima kufanyike vitu vya ziada kuhakikisha unafanya vitu ambavyo vitakuwa vinapendwa na wale ambao wanaangalia kazi. Farid ametua Yanga kuongeza makali kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.