Chama: Tukiwakosa saaana mbili!

Saturday September 19 2020

 

By CHARLES ABEL

STAA wa Simba, Clatous Chama ameweka wazi kwamba lengo lao kwenye mechi za nyumbani katika Uwanja wa Mkapa ni kupiga mabao mawili mpaka matatu. Ikiwemo ya kesho dhidi ya Biashara.

Chama alisema mechi mbili walizocheza ugenini dhidi ya Ihefu na Mtibwa hazikuwa na soka la maana na matokeo ya kufurahisha sana kutokana na aina ya viwanja haswa ule wa Morogoro ambao alisisitiza kwamba hauna hadhi ya ligi kama ya Tanzania.

“Msimu ndio kwanza umeanza kwa hiyo tutahitaji kuwa na rekodi nzuri haswa kwenye uwanja wetu wa nyumbani, tunatakiwa kuwa tunashinda kuanzia mabao mawili mpaka mpaka matatu kwa kila mechi.

“Tutaifanyia kazi sana, nina uhakika tutapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu, hii itakuwa faida sana kwetu kwavile mechi ya mwisho na Mtibwa ilikuwa mbaya kwasababu ya uwanja ulikuwa mbaya sana na niliudhika sana, tuko kwenye wakati ambao tunaboresha Ligi ya Tanzania viwanja kama vile haviwezi kutusaidia kwa namna yoyote ile, tunahitaji kubadilisha ubora wa viwanja vyetu,” alisema Chama.

SVEN NA KAGERE

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck amefunguka kuwa hana tatizo lolote na mshambuliaji Medie Kagere lakini amesisitiza kuwa hatokuwa tayari kupangiwa kikosi na mtu yeyote

Advertisement

Kauli hiyo ya Sven imekuja katika muda ambao kumekuwa na mjadala juu ya kitendo chake cha kumuweka benchi, Kagere ambaye Mfungaji Bora wa Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo iliyopita.

Mfumo wa kocha huyo wa 4-2-3-1 umechangia kumnyima namba Kagere.

Advertisement