Beki Mbeya City ni chochoro

Friday January 17 2020

Beki Mbeya City ni chochoro-Mbeya City -Singida United -Ligi Kuu Bara-Meddie Kagere-safu ya ushambuliaji ya Simba-

 

By Charity James

SAFU ya ulinzi ya Mbeya City imeonekana kuwa uchochoro zaidi miongoni mwa klabu za Ligi Kuu Bara ikiruhusu idadi kubwa ya mabao ikifuatiwa na Singida United kwa utofauti wa mabao manne.
Hadi sasa Mbeya City ikiwa imecheza michezo 17 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 24 wakati Singida United ambayo imecheza michezo 16 imeruhusu mabao 20.
Wakati timu hizo zikiwa na idadi kubwa ya kuruhusu nyavu zao kutikiswa, Simba ndio imeonekana kinara wa upachikaji wa mabao ikifanya hivyo mara 31 katika mechi zake 15.
Ubora wa safu ya ushambuliaji ya Simba ambayo inaongozwa na Meddie Kagere, ambaye amepachika mabao 10 hadi sasa imeonekana kuwa tishio zaidi.
Kagera Sugar ambayo inakimbiza na Simba kwenye idadi ya mabao imeachwa nyuma kwa mabao 11 mpaka sasa. Kagera Sugar ina mabao 20 iliyokusanya kwenye mechi zake 17 huku Yusufu Mhilu.

Advertisement