Azam kambi siku sita Zimbabwe kabla ya Triangle

Saturday September 21 2019

 

By DORISI MALIYAGA

KIKOSI  cha Azam FC kinatarajia kuweka kambi ya siku  sita Zimbabwe kabla ya kuivaa Triangle United ya nchini humo na wachezaji 18, wataondoka kesho Jumapili na ndege ya Shirika la ATCL.
Azam inakwenda huko tayari kwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupoteza nyumbani wiki iliyopita.
Na katika kupata matokeo mazuri, ndio maana wameamua kuivamia mapema Zimbabwe kwa ajili ya maandalizi zaidi kabla ya mchezo.
Ambapo baada ya kuondoka wataweka kambi ya siku tatu Harare na siku tatu nyingine watakaa Bulawayo kabla ya kucheza na Triangle.
"Lengo ni kufanya maandalizi mazuri ndio maana tumeamua kwenda Zimbabwe mapema. Kuna watu wametangulia kwa ajili ya kuweka mambo sawa ili timu itakapofika iwe salama,"alisema msemaji wa klabu hiyo, Jafar Idd.
Aliweka wazi, msafara utakaoondoka kesho ni wachezaji 18 na kocha msaidizi Idd Cheche ambao watakuwa Harare kwa siku tatu na  baadaye wachezaji wengine sita wataungana na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije watahamia Bulawayo.
Etienne na nyota hao watano Shaban Idd, Frank Domayo, Salum Abubakar 'Sure Boy', Idd Nado na Mudathir Yahya  

Advertisement