Aguero kuiwahi Wolves

Monday September 14 2020

 

London, England. Manchester City inaamini kuwa Sergio Aguero atakuwa fiti kuivaa Wolves katika mchezo wao wa kwanza.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye miaka 32, alifanyiwa upasuaji wa goti Juni, alitarajiwa kukosa michezo ya awali ya msimu mpya.
Lakini amekuwa na maendeleo mazuri katika kupona kwake na sasa anaweza kuwa uwanjani kukitumikia kikosi cha kocha Pep Guardiola katika mchezo wao dhidi ya Wolves wa Septemba 21.
Mtandao wa SunSport uliandika kuwa Aguero kwa sasa hana maumivu na anaendelea vizuri katika mazoezi mepesi.
Man City inaamini inaweza kumtumia katika mchezo huo mgumu wiki hii, ikiwa ni moja ya taarifa njema.
Kikosi cha kocha Guardiola kitaanza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England wiki moja baada ya timu nyingine kuanza, sambamba na Manchester United.
Hiyo inatokana na kuchelewa kumaliza msimu uliopita wiki tatu zilizopita baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Lyon.

Advertisement