United kuanza kukinukisha leo

Saturday September 19 2020

 

By MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya pazia la Ligi Kuu, England kufunguliwa wiki iliyopita, kivumbi kitaendelea tena leo kwa michezo minne kupigwa ambapo Manchester United itakuwa inacheza mchezo wake wa kwanza wa ligi dhidi ya Crystal Palace.
Kocha wa United Ole Gunnar Solskajer amezungumzia maandalizi ya mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 1:30 usiku kwa kusema wachezaji wake wapo tayari kiakilili na kimwili kupigana ili kupata matokeo, lakini atakuwa anawakosa baadhi ya wachezaji ikiwa pamoja na Phil Jones na Axel Tuanzebe hivyo kinda Teden Mengi ataendelea kuwepo katika safu ya ulinzi.
"Ni kweli tunahitaji ushindi na wachezaji wote wanahitaji kucheza, lakini utimamu wao wa kimwili haupo sawa hivyo nitawatumia wale ambao watakuwa sawa,"alisema Ole
Crystal Palace inaingia katika mchezo huo ikiwa inashika nafasi ya saba baada ya kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya Southampton bao 1-0.
Everton itakuwa inaumana na West Bromwich Albion mchezo utakaofanyika saa 8:30 mchana, huku Leeds United inayonolewa na Marcelo Bielsa itaivaa Fulham katika mchezo utakaopigwa saa 11:00 jioni.
Arsenal ikiwa nyumbani itaialika West Ham United katika Derby ya Jiji la London, mchezo huo utachezwa saa 4:00 usiku.

Advertisement