Tizi la Yanga, Simba wajipange

HILO tizi la Yanga usipime. Kocha Luc Eymael amezidi kuwapa dozi wachezaji wake, huku akitumia zaidi kuimarisha eneo la kiungo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuna siri kubwa kocha amegundua kwa wapinzani weo na hilo linawapa jeuri.

"Yanga ina rekodi ya kipekee kwenye michezo ya dabi ndio maana linatupa jeuri na wachezaji wote wapo kwenye morali ya hali ya juu.

"Kocha anataka viungo ndio wacheza zaidi kuliko safu nyingine, hayo ndio mazoezi ya leo, wachezaji wapo vizuri wanajituma kwa bidii kila mmoja unamuona ana hamu ya kushinda mechi hiyo,"

Ameongeza kuwa "Hatuna cha kupoteza dhidi ya Simba, tukishinda tutakuwa tunaendeleza rekodi zetu za kuwafunga mara nyingi, kuchukua mataji mara nyingi, hivyo wao ndio wana presha na mchezo huo,"amesema.

Amesema anaamini burudani itakuwa na mvuto wa hali ya juu kutokana na namna kocha ambavyo anakinoa kikosi hicho, mashabiki wa Yanga waje wengi kwani watafurahia kazi za vijana wao,"amesema.