Mkenya kulamba dili Pamba Jiji
Muktasari:
- Baraza aliyejiunga na Pamba Jiji Julai 31, 2025, alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kukifundisha TP Lindanda, unaofikia tamati msimu wa 2025-2026, ambapo yanafanyika mazungumzo ya kuongeza mwingine.
UONGOZI wa Pamba Jiji umeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba kocha wake Mkenya Francis Baraza baada ya kuridhishwa na kiwango cha timu hiyo hadi sasa Ligi Kuu Bara.
Baraza aliyejiunga na Pamba Jiji Julai 31, 2025, alisaini mkataba wa mwaka mmoja wa kukifundisha TP Lindanda, unaofikia tamati msimu wa 2025-2026, ambapo yanafanyika mazungumzo ya kuongeza mwingine.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Pamba Jiji (CEO), Peter Juma Lehhet alisema suala lolote linalohusu maboresho ya kikosi hicho iwe ya wachezaji au benchi la ufundi yatafanyika baada ya msimu huu wa 2025-2026, kumalizika.
“Tumeanza kuangalia maeneo ya kuboresha kwa ajili ya msimu ujao lakini ni mapema kwa sababu tuna mechi tatu zilizobakia ambazo tunataka tuzimalize vizuri, kisha baada ya hapo tufanye tathimini ya kina na benchi la ufundi,” alisema Lehhet.
Kwa upande wake Baraza alisema licha ya mwenendo mzuri wa timu hiyo msimu huu, ila bado wana-paswa kuongeza ushindani kwa mechi tatu zilizobakia, hivyo suala la kuzungumzia mkataba mpya ni mapema na anasubiria baada ya msimu huu kumalizika.
“Baada ya msimu kuisha nitakuwa na wakati mzuri wa kuzungumzia hilo kwa sasa akili zetu ni kumalizia kwanza mechi zote zilizobakia, kwangu nafurahia kufanya kazi na timu hii kutokana na ushirikiano nina-oendelea kuupata,” alisema Baraza.
Kocha huyo amewahi kuzifundisha Biashara United, Kagera Sugar na Dodoma Jiji za Tanzania huku aki-zifundisha Sony Sugar FC, Chemelil Sugar FC, Western Stima FC, Muhoroni Youth FC, Tusker FC na Ken-ya Police FC za Kenya kwa misimu mbalimbali.
Tangu Baraza ajiunge na Pamba Jiji, Julai 31, 2025, ameiongoza katika mechi 27, za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, ambapo kati ya hizo ameshinda tisa, sare tisa na kupoteza tisa, huku kikosi hicho kikiwa nafasi ya saba na pointi 36.