Uwanja wa Simba Bunju kumenoga, Yanga umnafeli wapi

Muktasari:

Katika hatua nyingine uwanja huo, mbali ya kuwepo wenye nyasi asilia lakini upo ambao utawekwa nyasi bandia.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’, ameendelea kuijenga timu hiyo kuwa imara kwa kuhakikisha Uwanja wa Bunju Complex unakamilika haraka iwezekanavyo.
kwenye uwanja huo ulipo Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  na kushuhudia hatua ambayo uwanja huo umefikia, ikiwa ni hatua za mwisho kabisa kabla ya kuanza kutumika.
Awali wakati uongozi ukiweka jiwe la msingi, Mo Dewji uliahidi uwanja huo utaanza kutumika kwa ya timu kuanzia mwezi Oktoba.
Kocha wa Simba Patrick Aussems alitembelea uwanja huo na kueleza Mo Dewji na uongozi wake wamefanya jambo kubwa huku akiridhishwa na hatua iliyofikiwa na kubaini umefanywa uwekezaji mkubwa  utakaokwenda kusaidia masuala ya kiufundi ndani ya timu na kufikia malengo yake.
“Ni kitu kikubwa hiki kimefanyika kwa Simba, kutokana na ukubwa wake, lingekuwa si jambo sahihi kukosa uwanja wa mazoezi kama huu ambao unaendelea kujengwa hapa.”
“Niwapongeze uongozi wa Simba chini ya Mo Dewji, lakini litakuwa jambo zuri zaidi wakikamilisha ujenzi huu kwa kila kitu kwa wakati na kabla ya ligi kuanza mzunguko wa pili timu iwe inatumia hapa kufanya mazoezi. “Simba ina wachezaji 30, kwa chumba cha kubadilishia nguo ambavyo nimekiona kitakuwa kidogo hivyo natamani waboreshe ili waongeze kiwe kikubwa au kujenga kingine.”
“Eneo la kuchezea nyasi zinaota ni nzuri na kama zitakuwa na matunzo katika hali ile nadhani utakuwa uwanja bora ambao tutatumia kwenye mazoezi yetu ya kila siku na kucheza mechi za kirafiki zile za kawaida.”
“Mambo mengine yote nimeyaona yamekwenda vizuri na tunasubiri tu muda wa kuutumia kwani nina imani hata wachezaji wangu wanatamani hilo,” aliongezea Aussems ambaye jana asubuhi  aliendelea kukinoa kikosi chake viwanja vya Gymkhana.
Msimamizi wa uwanja huo Richard Robert, alisema maendeleo ya viwanja vyote viwili ni mazuri tofauti na walipokuwa wameanza.
Alisema uwanja wenye nyasi asilia wapo hatua ya mwisho kwa maana ya kukata nyasi ambazo zipo wakati huu na kusubiri nyingine ziote ambazo zitakuwa tayari kutumika. “Maendeleo ya uwanja huu wa nyasi asili utakuwa tayari na kuanza kutumika wiki ya kwanza  ya mwezi Oktoba kwa maana ya kufanya mazoezi na kucheza zile mechi za kirafiki za kawaida,” alisema.

NYASI BANDIA
Katika hatua nyingine uwanja huo, mbali ya kuwepo wenye nyasi asilia lakini upo ambao utawekwa nyasi bandia.
Robert alisema uwanja wa nyasi bandia kesho Ijumaa, ndio wataweka nyasi hizo na zitachukua wiki mbili mpaka tatu kukamilika na kuanza kutumika.
“Kijumla maendeleo ya hapa Bunju Complex ni mazuri na makubwa ambayo viwanja vyote viwili nyasi bandia na asili vitatumika mwezi ujao.
“Baada ya kumaliza viwanja kwa maana maeneo ya kucheza na chumba cha kwanza kubadilishia nguo ambavyo ndani yake kuna vyoo na mabafu tutahamia maeneo ya nje kwa maana ya hosteli, gym, mabwawa ya kuogelea na mambo mengine ya msingi,” alisema.