Mreno Sofapaka aanza kuchora

Sunday September 1 2019

Mreno Sofapaka, Mwanapoti, Kenya, Tanzania aanza kuchora, Gor Mahia

 

By THOMAS MATIKO

LICHA wa kuwa na wiki tatu tu toka alipotua nchini kuwafunza Sofapaka, Kocha Mreno, Divaldo Alves ashaanza kuchora.
Alves tayari kadai anao ufahamu mzuri wa staili ya kila kocha aliye kwenye ligi kuu wa msimu huu inayoanza rasmi wikendi hii. Alves ataanza kibarua chake dhidi ya Posta Rangers inayofunzwa na kocha Sammy ‘Pamzo’ Omollo aliyeridhi mikoba hiyo wiki iliyopita kutoka kwake kocha John Kamau.
Kulingana na Alves, kando na kukiivisha kikosi chake, amekuwa akifanya utafiti sana kuhusiana na mbinu  za uchezaji wa makocha wa KPL na tayari ana ufahamu mzuri hivyo atakuwa akitumia habari hizo kuwasumbua.
Akianza na kibarua cha kesho dhidi ya Posta Rangers, Alves ambaye kasema mtindo wake utakuwa wa kimashambulizi zaidi akitilia nguvu zake kwenye mawing’a na mastraika, alisema tayari anayo kopi ya kocha Pamzo.
“Nawafahamu Ragers kutokana na nilichokisikia kwamba wana kocha mpya ambaye anapendalea timu yake kucheza difensi sana. Mara nyingi anapenda kuwa na wachezaji wengi nyuma akisubiria fursa ya kufanya shtukizi. Yupo tofauti na mtangulizi wake John Kamau ambaye naambiwa anapendelea soka la umilikaji wa mpira huku akishambulia sana. Taratibu nimekuwa nikizikusanya mbinu za makocha ili niweze kujua cha kufunya ninapokutana nao” Alves kasema. Alves aidha kasisitiza katika kikosi chake, hatakuwa na First 11 ila kwenye mechi atampanga mchezaji  anayemfurahisha mazoezini.
Sofapaka wana wachezaji 12 wapya baada ya kuwapoteza kadhaa waliounda kikosi cha kwanza ni ni matumaini yake kwamba watajeli haraka iwezekanavyo kabla ya ligi kufika mbali.

Advertisement