Ngao ya Jamii yarudishwa kwa Mkapa

MCHEZO wa Ngao wa Jamii kati ya Simba na Azam sasa utafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Samora Iringa lakini ghafla Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limebadili uwanja na kupangwa uchezwe Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo  ambao huwakutanisha bingwa wa Ligi Kuu Bara na bingwa wa Kombe la Shirikisho(FA) utaanza saa 1:00 usiku na TFF tayari imetangaza viingilio  ambayo ni VIP B na C  Sh10000 wakati mzunguko ni Sh 5000.
Simba tayari imeanza kujiwinda dhidi ya Azam baada ya kurejea nchini juzi ikitokea Msumbiji ilipocheza mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Azam inatarajiwa kurejea leo Jumatatu ikitokea Ethiopia ilikokuwa ikicheza mchezo wa Kombe la la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema na kuambulia kipigo cha bao 1-0.
Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema sababu kubwa za kuhamisha uwanja ni kutokana na sababu sa kiufundi.