Beckham mawazo tele kwa Messi, Ronaldo

Saturday February 29 2020

 

MIAMI, MAREKANI .DAVID Beckham amekiri kuvutiwa na mpango wa kuwanasa masupastaa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kwenye kukipiga kwenye timu yake ya Inter Miami.
Klabu hiyo ya Beckham inaanza kucheza msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Marekani mwaka huu. Akiwahi kuwa mchezaji mkubwa kwenye soka, ambapo alitamba na klabu za Manchester United na Real Madrid kwa kuzitaja kwa uchache, mpango wa Beckham ni kuvuta mastaa wenye majina makubwa kwenye klabu yake hiyo ya Miami.
Na amekiri kwamba angependa kuwanasa mastaa kama Ronaldo na Messi kwenye kucheza kwenye timu yake.
"Tunafurahia kwa orodha iliyopita, wachezaji waliopo, lakini nafirahia pia kama tunazungumzia uwezekano wa kuwachukua wachezaji wakubwa kutoka Ulaya kuja kucheza kwenye timu yetu," alisema.
"Kila timu duniani ingehitaji kuwa na huduma ya Messi na Ronaldo kwenye vikosi vyao. Lakini, siku zote tumekuwa tukijizungumzia sisi kuwa timu tofauti na nyingine, kitu ambacho naamini hata waamini wa klabu nyingine nao watakuwa wanasema kitu kama hicho.
"Hivyo basi tunajaribu jambo hilo na kama tutakuwa na nafasi ya kuleta mastaa wakubwa kwenye timu itakuwa bahati yatu na tunataka kufanikiwa hivyo tunahitaji kuleta wachezaji bora."
Beckham aliwahi kuzichezea pia AC Milan, Paris Saint-Germain na LA Galaxy katika maisha yake ya soka.

Advertisement