Azam yaipania Kagera Sugar

Saturday March 23 2019

 

By THOMAS NG’ITU

KIKOSI cha Azam kimeendelea na mazoezi yake kukijiandaa na mchezo wao wa Kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar, lakini katika mazoezi hayo kocha Idd Cheche aliwapa wachezaji wake mazoezi maalumu ya kuimaliza mapema Kagera Sugar. Katika mazoezi hayo, Cheche aliwachezesha wachezaji wake nusu uwanja kisha aliweka magoli matatu na kutaka kila goli wachezaji hao waweze kukaba na kushambulia.

Zoezi hilo lilikuwa halimwachi mchezaji kusimama akiwa huru badala yake ilimlazimu kukaba na kushambulia kwa wakati mmoja kutokana na eneo dogo walilokuwa wakilitumia. Cheche aliliambia Mwanaspoti kuwa kwa mazoezi anayowapa wachezaji wake, anaamini wataibuka na ushindi katika mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Advertisement