Mendy anakula mkwanja mrefu benchi Man City

Saturday August 17 2019

 

MANCHESTER, ENGLAND. BEKI wa kushoto wa Manchester City, Benjamin Mendy walau yupo kwenye hatua nzuri za kupona majeruhi yake baada ya kuigharimu pesa nyingi zake klabu yake hiyo kutokana na kukaa tu kwenye benchi.
Beki huyo amekuwa nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti ambayo yalimfanya afanyiwe upasuaji. Mendy alikuwa huko Barcelona akijiuguza, lakini sasa amerudi jijini Manchester kujiunga na wenzake kwa ajili ya mazoezi.
Man City hawana haraka ta kumfanya Mendy kurudi uwanjani licha ya kwamba kwamba amewagharimu pesa nyingi kwa kuendelea kukaa tu kwenye benchi. Mendy amekumbwa na majeruhi ya goti siriazi mara mbili tangu alipojiunga na Man City akitokea Monaco kwa ada ya Pauni 49.3 milioni Julai 2017. Lakini, kwa sasa anapambana kurudi uwanjani kabla ya mapumziko ya mechi ya kirafiki mwezi ujao.
Kwenye kikosi cha Man City, nafasi ya Mendy kwa sasa kaishilia Oleksandr Zinchenko na huduma ya beki huyo imemfanya kupewa mkataba mpya hivi karibuni. Kwa kipindi cha miaka miwili, Mendy amekosa zaidi ya mechi 90, huku katika kipindi hicho amelipwa mshahara wa Pauni 10.4 milioni, ambapo ni sawa na Pauni 2.6 milioni Man City imemlipa katika kila mechi ambacho amekuwa tu benchi.
Kwa kuchukua dakika 1,721 alicheza katika mechi 23, hiyo ina maana kwamba Mendy amelipwa Pauni 35,000 kwa kila dakika. Lakini, wakati Mendy akijiandaa kurudi uwanjani, staa mwenzake kwenye kikosi hicho Leroy Sane atakuwa benchi kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Liverpool wiki mbili zilizopita. Kocha, Pep Guardiola alisema kwamba ana wasiwasi Sane atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana kutokana na majeruhi hayo ambayo pia yamemtibulia dili lake la kwenda kujiunga na Bayern Munich.

Advertisement