Ndinga hili tishio jipya mbio za magari MAFANIKIO yaliyoletwa na Kampuni ya magari ya Toyota kutokana na ubora wa gari lao aina ya Toyota R5, yamewapa mzuka madereva wa mbio hizo kutaka kuendelea nayo katika mashindano yajayo.
Lina Tour sasa kuanzia Moro RAUNDI ya kwanza ya michuano ya Lina Tour kwa mwaka huu inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Gymkhana, mjini Morogoro na si Arusha kama ilivyotangazwa awali. Kabla ya mabadiliko haya...
FIA yaipa Tanzania raundi ya tano ya ARC CHAMA cha mchezo wa mbio za magari duniani, FIA kimetoa kalenda mpya ya mbio za magari ubingwa wa Afrika na Tanzania itaandaa raundi ya tano na si ya nne kama ilivyotangazwa awali.
Madina, Vicky wakwama gofu Sauzi NYOTA wa Tanzania, Madina Iddi na Vicky Elias wameambulia patupu kwenye mashindano ya gofu ya mashimo 36 ya R&A yaliyofanyika Afrika Kusini, mmoja akimaliza nafasi ya 14 huku mwingine akijitoa.
Tanzania ipo tayari kupindua meza KUSHINDA mechi ya ufunguzi wa michuano ya ICC League B dhidi ya Italy na tatu nyingine zinazofuata, ndio azma kuu ya timu ya Tanzania katika ligi hii kimataifa inayoanza kuchezwa rasmi ijumaa hii...
Madina, Vicky mguu sawa Sauzi MADINA Idd na Vicky Elias wamedai zoezi ya kuzisoma changamoto za viwanja vya Leopards Creek, Mpumalanga, Afrika Kusini linaendelea vyema kabla ya michuano ya gofu ya wanawake wa Afrika kuanza...
Mount Uluguru kidedea tuzo za madereva KLABU ya mbio za magari ya Mount Uluguru imetwaa taji la klabu bora ya mwaka 2024 na kupewa tuzo maalum katika hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika mwishoni mwa juma katika Hoteli ya Golden...
Mbio za mita 3000 kiunzi kirefu miaka 45 MBIO za mita 3000 kuruka viunzi na maji (steeplechase) zimekuwa ni mtihani usio na majibu kwa miaka 45 sasa tangu Filbert Bayi azitumie kuipatia Tanzania medali ya fedha katika michuano ya...
KO ya Mama imefichua ukweli NGUMI za kulipwa ndio mchezo ulioifuatia soka kwa ubora mwaka 2024, na wadau wa michezo wanahofu michezo mingine kuendelea kudorora wakati soka ikidaiwa itazidi kuongoza kwa kutoa ajira 2025.
Gymkhana kumekucha na Lina PG Tour RAUNDI ya tano ya Linar PG Tour inatarajiwa kuanza leo kwenye viwanja vya Dar Gymkhana, kuhitimisha michuano ya gofu ya mwaka huu, huku mshindi akiondoka na Sh8.8 milioni.