Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xavi Simons akija kuna mtu anatoka

XAVI Pict

Muktasari:

  • Chelsea imekuwa bize sana kwenye dirisha hili la usajili na sasa ina pesa ya kusajili baada ya kumuuza Noni Madueke kwenda Arsenal.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA ipo kwenye hatua za mwisho kabisa kunasa saini ya Xavi Simons, lakini dili hilo litamshuhudia staa mmoja wa Chelsea akichomolewa kikosini.

Chelsea imekuwa bize sana kwenye dirisha hili la usajili na sasa ina pesa ya kusajili baada ya kumuuza Noni Madueke kwenda Arsenal.

Madueke alijiunga na Arsenal kwa ada ya Pauni 52 milioni, hivyo kuifanya Chelsea kuwa na pesa za kutosha kunasa saini ya staa wa RB Leipzig, Simons, ambaye anaweza kuwagharimu Pauni 60 milioni.

Makubaliano binafsi yanaripotiwa kuwa hatua za mwisho kufikiwa na mkali huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo tayari kutua Stamford Bridge.

Hata hivyo, kwenye dili hilo la Simons, linaweza kumshuhudia mchezaji Carney Chukwuemeka akitoka Stamford Bridge kwenda Leipzig ikiwa ni mpango wa dili la kubadilishana wachezaji.

Simons alifunga mabao 10 na kuasisti saba kwenye mechi 25 alizocheza kwenye Bundesliga msimu uliopita na aliwahi kuhusishwa na Arsenal.

Leipzig inaripotiwa kwamba ipo tayari kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Uholanzi.