Xabi Alonso apuuzia ishu ya Madrid
Muktasari:
- Kiungo hiyo wa zamani wa Los Blancos, Alonso, 41, amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kuinoa klabu hiyo ya Bernabeu kwa zaidi ya miezi 12 sasa iliyopita baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika kibarua chake cha kuinoa Bayer Leverkusen msimu uliopita.
MUNICH, UJERUMANI: KOCHA Xabi Alonso ameupuuzia uvumi unaodai kwamba atakwenda kuwa kocha mpya wa Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo hiyo wa zamani wa Los Blancos, Alonso, 41, amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kuinoa klabu hiyo ya Bernabeu kwa zaidi ya miezi 12 sasa iliyopita baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika kibarua chake cha kuinoa Bayer Leverkusen msimu uliopita.
Ripoti za Alonso kwenda kuchukua mikoba ya kuinoa Real Madrid zimeongezeka kwa siku za karibuni baada ya Kocha Carlo Ancelotti kuwa tayari kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, ambako Mtaliano huyo akitaka kwenda kukabiliana na changamoto mpya kwingineko.
Lakini, Alonso ameamua kuzipuuzia taarifa hizo na kufichua kwa sasa akili yake ipo kwenye kupambania kibarua chake huko Bayer Leverkusen.
“Kuna swali la Real Madrid? Muda unakwenda na mambo yabakia,” alisema Alonso na kuongeza. “Uhusiano wetu umeimarika, lakini akili yangu kwa sasa nimeielekeza Bayer Leverkusen, hilo ndilo lililopo akilini mwangu.”
Alonso na Ancelotti mikataba yapo kwenye klabu zao itafika tamati 2026. Hata hivyo, makocha hao wawili wote wapo tayari kuachana na timu zao kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.