William Saliba, Real Madrid ndo basi tena
Muktasari:
- Inaelezwa Madrid iliona Arsenal inahitaji huduma ya Rodyrigo, hivyo ikatumia fursa hiyo kutaka kufanya mabadilishano wawape staa huyo ili wao wamchukue Saliba, jambo ambalo limekataliwa na washika mitutu hao.
LONDON, ENGLAND: REAL Madrid inadaiwa kukwama katika mpango wao wa kutaka kumsajili beki kisiki wa Arsenal William Saliba baada ya ofa yao ya kutaka kufanya mabadilishano ya wachezaji kukataliwa na klabu yake.
Inaelezwa Madrid iliona Arsenal inahitaji huduma ya Rodyrigo, hivyo ikatumia fursa hiyo kutaka kufanya mabadilishano wawape staa huyo ili wao wamchukue Saliba, jambo ambalo limekataliwa na washika mitutu hao.
Awali iliripotiwa Madrid inataka kusubiri hadi mwaka 2027 mkataba wake utakapomalizika ili imsajili bure au dirisha la majira ya kiangazi mwakani na inaamini ingempata kwa bei nafuu.
Hata hivyo, baada ya kuona kuna fursa ya kumpata kwa mabadilishano, Madrid ilijaribu kuwasilisha ofa.
Mapema mwaka huu, staa huyu alipoulizwa kuhusu mustakabali wake alisema: "Kwangu, nina furaha kweli kuendelea kuwa hapa. Nimekuwa hapa kwa miaka miwili na nusu. Hakuna kitu juu ya tetesi zinazoendelea. Nina furaha hapa na nataka kuendelea kubakia."
"Nataka kushinda mataji makubwa nikiwa na Arsenal. Ukiondoka kwenye timu bila kushinda chochote mashabiki watakusahau. Nataka kushinda mataji kwanza."
Beki huyu wa kimataifa wa Ufaransa pia aliulizwa kama kulikuwa na mazungumzo kuhusu mkataba mpya na Arsenal, alijibu: "Bado. Nafikiri ni mapema sana, tuna miaka kadhaa imebakia kwenye mkataba. Hivyo basi hakuna haraka kwa sasa."
Alipoulizwa juu ya hilo, Kocha Mikel Arteta alisema: "Naliacha suala hilo kwa mabosi wa timu, kipaumbele changu kikuu ni kuhusu utendaji tu, kuandaa mbinu na kushinda mechi kwa sababu sasa tumeshaanza msimu.