Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili watia presha Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • White hakuwapo kwenye mazoezi ya wazi huko London Colney, wakati Zubimendi alionekana kufanyiwa uchunguzi akiwa nje ya uwanja wa mazoezi ambapo mkurugenzi wa michezo Andrea Berta, naye alikuwapo.

LONDON, ENGLAND: MASTAA Martin Zubimendi na Ben White wanampa presha kocha Mikel Arteta baada ya kudaiwa kuwa majeruhi wakati kikosi cha Arsenal kikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Fulham.

White hakuwapo kwenye mazoezi ya wazi huko London Colney, wakati Zubimendi alionekana kufanyiwa uchunguzi akiwa nje ya uwanja wa mazoezi ambapo mkurugenzi wa michezo Andrea Berta, naye alikuwapo.

Kuna habari njema kwa kocha Arteta, kwamba mchezaji Piero Hincapie alishiriki vyema mazoezi. Staa huyo aliyesajiliwa siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi alicheza dakika chache tangu aliponaswa kutoka Bayer Leverkusen kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya kinena na alikuwa nje ya uwanja kwa mechi tano zilizopita.

Ishu ya utimamu wa mwili imekuwa tatizo kwenye kikosi cha Arsenal msimu huu, ambapo William Saliba, Bukayo Saka na Martin Odegaard, ambao wamekosa mechi kadhaa msimu huu kutokana na matatizo mbalimbali. Odegaard kwa sasa yupo nje ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti ambapo hatacheza hadi Novemba.

ARS 01
ARS 01

Nahodha huyo wa Arsenal alishakosa mechi kadhaa mara mbili tofauti msimu hu kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega na alikuwa na maumivu ya goti aliyopata kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa za Oktoba.

Noni Madueke na Kai Havertz nao wanatarajia kurudi uwanjani mwezi ujao, huku kocha Arteta akiamini staa wake wa Kijerumani, Havertz anaweza kurudi uwanjani hivi karibuni.

Saka na Saliba walicheza kwa viwango bora katika timu zao za taifa, wakionekana kuwa kwenye ubora unaotosha kuanza dhidi ya Fulham. Jurrien Timber amekuwa na kiwango bora kwenye beki ya kulia, hivyo White kukosekana haitakuwa tatizo, lakini ishu ipo kwa Zubimendi.