Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakala wa Wirtz atoa kauli nziti kumuhusu Xabi Alonso

Muktasari:

  • Licha ya kupitia mwanzo mgumu katika maisha ya Ligi Kuu England kufuatia uhamisho wake wa Pauni 116 milioni kutoka Bayer Leverkusen kwenda Liverpool, Wirtz hivi karibuni ameanza kuonyesha kiwango kizuri.

LIVERPOOL, ENGLAND: WAKALA wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Florian Wirtz, Volker Struth, ametoa kauli nzito kuhusu kocha Xabi Alonso alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Licha ya kupitia mwanzo mgumu katika maisha ya Ligi Kuu England kufuatia uhamisho wake wa Pauni 116 milioni kutoka Bayer Leverkusen kwenda Liverpool, Wirtz hivi karibuni ameanza kuonyesha kiwango kizuri.

Mjerumani huyo alihitaji kusubiri hadi Desemba, 27, mwaka jana kwa ajili ya kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu England akiwa na Liverpool ambalo alifunga dhidi ya Wolves.

Tangu wakati huo, Wirtz amefunga mabao mengine matano na kutoa asisti nane za mabao katika mechi 35 alizocheza.

Ingawa inaonekana Wirtz ameanza kuzoea maisha ya viunga vya Anfield, wakala wake Struth amefichua jambo la kushangaza kuhusu dili lake la kutua Liverpool.

Bayern Munich na Manchester City zote zilionyesha nia ya kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 22, lakini Liverpool ndio iliyoshinda vita.

Hata hivyo, Struth sasa amedai kuwa aliwasiliana na rais wa Real Madrid, Florentino P rez, kuhusu uwezekano wa Wirtz kuhamia Santiago Bernabeu.

Akizungumza na chombo cha habari cha Ujerumani Bild, wakala huyo alisema: "Katika kipindi ambacho uhamisho wa kwenda Liverpool au Bayern ulikuwa unajadiliwa, nilimpigia simu Xabi Alonso na kumwambia: "Lazima umchukue huyu kijana uende naye Madrid."

Alonso alijiunga na Madrid kutoka Leverkusen katika majira ya kiangazi mwaka 2025, baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na Leverkusen.

"Xabi alinijibu: 'Huna haja ya kuniambia mimi, unapaswa kumwambia Florentino Perez.'

"Kwa hiyo nilimtumia ujumbe Florentino na kumwambia kwamba ningependa kuona Wirtz akijiunga nao."

Wakala huyo alieleza kuwa Perez aliupeleka ujumbe huo kwa mkurugenzi mtendaji wa Madrid, Sanchez, lakini dili hilo halikufanikiwa. Badala yake, mabingwa hao wa La Liga waliwasajili Trent Alexander-Arnold, Dean Huijsen, Alvaro Carreras na Franco Mastantuono.

"Mwaka huo, haikuwa wakati sahihi kutokana na kikosi na bajeti ya timu, kuna muda hata Madrid huwa hawana pesa za kutosha kusajili wachezaji."

Liverpool itarejea uwanjani nyumbani dhidi ya West Ham United Jumamosi Februari, 28, na Wirtz anatarajiwa kuwamo kikosini.