Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakala amtishia Udogie bastola

Muktasari:

  • Mchezaji huyo anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 60 milioni alikumbana na tukio hilo la kutishiwa bastola wakati akiwa kwenye matembezi mitaa ya London.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Tottenham Hotspur, Destiny Udogie ametajwa kuwa ni mwanasoka wa Ligi Kuu England aliyetishiwa bastola na wakala wake.

Mchezaji huyo anayetajwa kuwa na thamani ya Pauni 60 milioni alikumbana na tukio hilo la kutishiwa bastola wakati akiwa kwenye matembezi mitaa ya London.

Msemaji wa klabu ya Tottenham Hotspur alisema: “Tunampatia sapoti Destiny na familia yake kwa tukio lililotokea na tutaendelea kufanya hivyo. Kutokana na jambo hilo lipo kwenye mikono ya kisheria, hatuwezi kusema vitu vingi zaidi ya hivyo.”

Maofisa wa polisi wanaripotiwa kumkamata wakala huyo, mwenye umri wa miaka 31, baada ya kuripotiwa kuzua taharuki kwa Udogie na familia yake kwa kuwatishia kwa bastola katika tukio lililotokea mtaani Septemba 6.

Kinachoelezwa ni kwamba hilo limetokana baada ya mchezaji kusitisha kufanya kazi na wakala huyo. Wakala huyo anafanyiwa uchunguzi kwa sasa juu ya madai ya kutaka kumfanyia udanganyifu mchezaji pamoja na kumtishia bastola. Tukio hilo lilimtetemesha Udogie baada ya kuonyeshwa bastola, katika tukio ambalo alihofia uhai wake. Hata hivyio, Udogie alianzishwa kwenye mechi ya usiku wa Jumanne, ambapo Spurs iliangushia kipigo kizito Copenhagen kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Na alitumika pia kwenye mechi dhidi ya West Ham United. Udogie alijiunga na Spurs kwa ada ya Pauni 17.6 milioni akitokea Udinese mwaka 2022.