Wachezaji 15 wenye sura mbaya

dirk kuyt
LONDON, ENGLAND SOKA ni mchezo mzuri unaoiteka dunia, kutokana na hilo wachezaji nyota hupendwa bila kujali wana sura za aina gani. Wafuatao ni wachezaji wasio na sura za mvuto katika soka. 15.Dirk Kuyt: Liverpool, Uholanzi Anaweza kuigiza kama muhusika mkuu katika filamu za kutisha bila kuvaa kinyago. 14.Mario Balotelli: Man City, Italia "Kama ningekuwa rais ningetaka watu waishi vizuri, kama ningekuwa milionea ningenunua ndege binafsi, kama ningekuwa mnyama ningechagua kuwa simba na kama ningekuwa Mario Balotelli ningechagua kuwa mtulivu na ningenyoa nywele vizuri." Hiyo ni kwa sababu Mario hana sura nzuri lakini angependeza zaidi kama angetulia. 13. Gareth Bale: Tottenham, Wales Watu waliojifunza historia ya Homo sapiens (yale mabadiliko ya nyani kuwa binadamu) wanaweza kumfananisha Bale na watu hao. 12.Taye Taiwo: Marseille, Nigeria Unaweza kusema anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa ngozi kwa kuwa sura yake haivutii. 11.Martin Skrtel: Liverpool, Slovakia Hivi huwa washambuliaji wanafanya nini kupambana na mtu huyo?...Nadhani wanaogopa. 10.Louis Saha: Everton, Ufaransa Ana nywele za rangi ya dhahabu ambazo haziendi sambamba na rangi ya ngozi yake, ningekuwa mshauri wake ningemkumbusha abadili na kuwa nywele nyeusi. 9.Bacary Sagna: Arsenal, Ufaransa Hana sura ya mvuto na kinachoongeza ubaya ni staili zake za nywele ambazo hazivutii kabisa. 8.Michael Essien: Chelsea, Ghana Anapendwa na wasichana kama Nadia Buari kutokana na uhodari wake lakini uso wake hauvutii sana. 7.Steve Sidwell: Aston Villa Watu kadhaa humwambia ukweli kuwa hana mvuto, lakini ana mke mzuri aitwaye Krystell pamoja na watoto wawili. 6.Gerald Asamoah: St. Pauli Mashabiki wa Ujerumani wamekuwa wakimuita sokwe, si kweli kuwa ni soke ila sura yake si njema sana. 5.Dominic Adiyiah: Reggina, Ghana Ni shujaa wa taifa lake ambaye mpira wake uliokolewa na Luis Suarez kwa mkono katika fainali za Kombe la Dunia 2010. Wengi humwambia havutii. 4.Wayne Rooney: Man United, England Hivi unaweza kuwa na furaha kuzaa mtoto anayefanana na Wayne Rooney? Havutii kimapenzi lakini anapendwa na wanawake kutokana na jitihada zake uwanjani 3.Carlos Tevez: Man City, Argentina Anafahamika kwa jina la mnyama. Hana mvuto, lakini ndio injini ya Man City. 2.Frank Ribery: Bayern Munich, Ufaransa Hashangai kuonekana hana mvuto. Nyota huyo aliungua na maji ya moto usoni wakati akiwa mdogo. 1.El Hadji Diouf: Blackburn Havutii wanawake wengi kwani ana tabia mbaya za uropokaji na ugomvi.