Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu warudi kwa Vinicius Jr

SALAH

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa Real Madrid amekuwa akiwindwa na matajiri hao wa Saudia tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya fundi huyo kukataa mwenyewe.

RIYADH, SAUDI ARABIA: INAELEZWA matajiri wa Saudi Arabia wamerudi mezani kuzungumza na wawakilishi wa Vinicius Jr ili kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa lengo la kuongeza ushawishi zaidi katika ligi yao.

Mchezaji huyo wa Real Madrid amekuwa akiwindwa na matajiri hao wa Saudia tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya fundi huyo kukataa mwenyewe.

Inaelezwa, matajiri hao wameweka mezani kiasi kisichopungua Euro 250 milioni kama ada ya uhamisho pamoja na mshahara mnono.

Licha ya ukweli siyo jambo la ajabu kwa timu za Saudia kutoa mishahara mikubwa, lakini inaelezwa kiasi ambacho wameweka kama ofa kwa Vinicius kinaweza kuvunja rekodi ya dunia.

Matajiri hao wanataka kutoa ofa nono kwa sababu wanaamini kumsajili winga huyo haitakuwa tu kama pigo kwa soka la Ulaya, bali ni hatua ya kimkakati ambayo itasaidia kuongeza ushawishi zaidi kwenye ligi yao.

Mashabiki wa Madrid wameonekana kugawanyika na baadhi wanataka timu yao ichukue pesa na kumuuza fundi huyo wa kimataifa wa Brazil na wengine wakisisitiza asizuwe kutokana na mchango wake mkubwa.

Licha ya ofa hiyo nono, hadi sasa hakuna uamuzi wowote uliotolewa na mabosi wa Madrid na ripoti zinaeleza kuna mazungumzo yanaendelea na kwa upande wa viuongozi pia wamegawanyika kuhusu abaki ao auzwe.