Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wanamtaka tena Bruno Fernandes

BACK Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa mashetani wekundu alikuwa akihitajika na Al-Hilal mapema katika dirisha hili la majira ya kiangazi ambapo iliwasilishwa ofa ya Pauni 200 milioni.

MANCHESTER, ENGLAND: AL Nassr ya Saudi Arabia imerudi tena mezani kutaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes katika dirisha hili ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kuikataa ofa ya kwanza kutoka Al-Hilal.

Nyota huyo wa mashetani wekundu alikuwa akihitajika na Al-Hilal mapema katika dirisha hili la majira ya kiangazi ambapo iliwasilishwa ofa ya Pauni 200 milioni.

Fernandes, mwenye umri wa miaka 30, alikataa ofa hiyo kubwa na akaonyesha nia ya kubaki katika Ligi Kuu  England.

Kwa mujibu wa gazeti la Ureno A Bola, klabu ya Ronaldo, Al-Nassr, sasa inafikiria kuwasilisha ofa kwa Fernandes.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 41, hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa miaka miwili wa kihistoria utakaomwezesha kukunja Pauni 492 milioni katika kipindi chote hicho.

Kama Fernandes atasajiliwa na Al Nassr, ataungana na mastaa wengine wa Ureno kama Ronaldo, Otavio, na Joao Felix ambaye ametua hivi karibuni.

Hata hivyo, licha ya ripoti hizo, inaonekana sio rahisi kwa nahodha Fernandes kubadili uamuzi wake wa kubaki Old Trafford na kuondoka kwa sasa. Akithibitisha uamuzi wake wa kubaki Man United Juni mwaka huu, Ferandes alisema: “Ingekuwa ni uamuzi rahisi, kuna wachezaji wenzangu raia wa Ureno kule ni Ruben Neves na Joao Cancelo kule Al-Hilal, watu ambao nina urafiki nao mkubwa. Lakini bado nataka kubaki kwenye soka la ushindani na  kucheza mashindano makubwa, kwa sababu bado najihisi kuwa na uwezo.

“Kulikuwa na nafasi ya kujiunga nao. Rais wa klabu alinipigia simu na kuniuliza kama nataka kwenda kule. Walikuwa wakinisubiri. Nilizungumza na Ruben Amorim akanisihi nisiondoke. Vilevile Man United hawakutaka niuzwe. Hawana shida ya pesa. Iwapo ningetaka kuondoka, wangeniruhusu.”

Hadi sasa Man U imeongeza nguvu kwa kuwasajili Bryan Mbuemo na Matheus Cunha kwa jumla ya Pauni 133 milioni. Pia, inaripotiwa kuwa inamuwania mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko.