Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vitinha aipa ubingwa wa dunia Ureno

VITINHA Pict

Muktasari:

  • Vitinha, aliyecheza Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, sasa anaingia kwenye mashindano ya 2026 akiwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa kikosi hicho chini ya kocha Roberto Marti­nez.

LISBON, URENO: KIUNGO nyota wa Paris Saint-Germain, Vitinha amesema kikosi chao cha timu ya taifa la Ureno kina kila kitu kinachohitajika kufanikisha ndoto ya kutwaa Kombe la Dunia 2026 huku akieleza kuwa mchanganyiko wa vijana na uzoefu ndani ya timu hiyo unaweza kuwa siri ya mafanikio yao.

Vitinha, aliyecheza Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, sasa anaingia kwenye mashindano ya 2026 akiwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa kikosi hicho chini ya kocha Roberto Marti­nez.

Kiungo huyo aliyeisaidia PSG kutwaa ubingwa wa tano wa Ligue 1 pamoja na Ligi ya Mabingwa msimu wa 2024/25 amesema anafurahia jukumu kubwa alilonalo ndani ya timu ya taifa ya Ureno.

VITI 01

Nina nafasi kubwa zaidi sasa ndani ya timu ukilinganisha na zamani. Nafurahia kuwa na majukumu hayo na ninajitahidi kufanya vizuri ili kuendana na matarajio,€  amesema Vitinha.

Nyota huyo amesema ana hamu kubwa ya kucheza Kombe la Dunia 2026 kwani itakuwa mara yake ya pili kushiriki mashindano hayo huku akitarajia kuwa na mchango mkubwa zaidi safari hii.

‘‘Nina hamasa kubwa sana kwa sababu natamani kucheza Kombe hili la Dunia. Natumaini kupata muda zaidi wa kucheza na kuwa na nafasi muhimu zaidi ndani ya timu”  amesema.

Ureno kwa sasa ina kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji wenye uzoefu na vijana wenye vipaji. Wachezaji wakubwa kama Bruno Fernandes, Bernardo Silva, Ruben Dias na Joao Cancelo wanaungana na kizazi kipya chenye nyota kama Rafael Leao, Pedro Neto pamoja na Joao Neves.

VITI 02

Pamoja na uwepo wa kizazi hicho kipya, bado timu hiyo inaendelea kuongozwa na nahodha mkongwe Cristiano Ronaldo ambaye anaendelea kucheza katika kiwango cha juu licha ya kutimiza miaka 41. Vitinha amesema uwepo wa Ronaldo ndani ya kikosi ni jambo kubwa kwa vijana wa timu hiyo kutokana na nidhamu na weledi wake.

‘‘Ni jambo la ajabu kushiriki naye vyumba vya kubadilishia nguo. Ronaldo ni mmoja wa wachezaji bora kabisa katika historia ya soka. Tunajifunza mengi kutoka kwake kila siku,’’ amesema.

Aliongeza kuwa kitu kikubwa alichojifunza kutoka kwa Ronaldo ni namna anavyojiandaa kwa umakini mkubwa kabla ya kila mchezo.

Ureno ambayo ipo Kundi K itacheza mechi yake ya kwanza katika Kombe la Dunia, Juni 17, 2026 dhidi ya DR Congo kwenye Uwanja wa NRG, Houston.