Vigogo Newcastle United wanaogopa
Muktasari:
- Liverpool, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, wameonyesha wako tayari kusitisha kwa muda nia ya kumsajili Isak baada ya ofa yao ya Pauni 110 milioni kukataliwa na Newcastle.
NEWCASTLE, ENGLAND: MABOSI wa Newcastle wana hofu kwamba Liverpool iko tayari kutumia mbinu ya kusubiri kama ile ilivyofanya kwa Virgil van Dijk ili kuhakikisha inainasa saini ya mshambuliaji Alexander Isak, ambaye thamani yake inakadiriwa kufikia Pauni 150 milioni.
Liverpool, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, wameonyesha wako tayari kusitisha kwa muda nia ya kumsajili Isak baada ya ofa yao ya Pauni 110 milioni kukataliwa na Newcastle.
Isak, raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 25, ametangaza nia ya kujiunga na Liverpool na kwa sasa anafanya mazoezi katika miundombinu ya klabu yake ya zamani, Real Sociedad, wakati wachezaji wenzake wa Newcastle wakiwa kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya barani Asia, safari ambayo hakushiriki kutokana na majeraha madogo ya paja.
Hali hiyo imeanza kumweka pabaya mbele ya mashabiki wa Newcastle licha ya kocha Eddie Howe kusisitiza kuwa mchezaji huyo bado ni mchezaji wa timu na anapata msaada kamili klabuni.