Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo Marekani wamgombania Casemiro

Muktasari:

  • Inaelezwa kwamba Casemiro yupo tayari hadi kuchukua mshahara wa chini ili tu apate nafasi ya kucheza Ligi Kuu Marekani kwani anawindwa pia na matajiri wa Saudi Arabia, lakini amekataa kwenda nchini humo.

LOS Angeles Galaxy na Inter Miami za Ligi Kuu Marekani zimeonyesha kuvutiwa na kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya Brazil, Carlos Henrique Casimiro maarufu Casemiro mwenye umri wa miaka 34 ambaye ametangaza kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa kwamba Casemiro yupo tayari hadi kuchukua mshahara wa chini ili tu apate nafasi ya kucheza Ligi Kuu Marekani kwani anawindwa pia na matajiri wa Saudi Arabia, lakini amekataa kwenda nchini humo.

Kwa sasa staa huyo anaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kujiunga na Inter Miami ya Lionel Messi ambayo ofa yake inaonekana kuwa ndogo ukilinganisha na timu nyingine zinazomtaka. Baadhi ya mashabiki wa Man United wamekuwa wakiimba wahitaka nyota huyo abaki kutokana na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Man United hususan msimu huu. Casemiro ambaye alijiunga na Man United 2022, msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote.


Rasmus Hojlund

NAPOLI ipo tayari kulipa pesa zinazotakiwa ili kumsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Manchester United, Rasmus Hojlund, 23, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa katika makubaliano ya mkataba wa kumsajili Rasmus kwa mkopo uliosainiwa dirisha lililopita, kulikuwa na kipengele kinachoeleza Napoli italazimika kulipa Pauni 38 milioni na kumsainisha mkataba wa kudumu ikiwa itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Crysencio Summerville

MMSHAMBULIAJI wa West Ham United, Crysencio Summerville, 24, anafuatiliwa kwa karibu na baadhi ya klabu kubwa Ulaya ambazo zimepanga kuwasilisha ofa ya kumsajili mara tu Ligi Kuu England itakapomalizika msimu huu. Inaelezwa klabu hizo zinaona kuwa zitakuwa na nafasi kubwa ya kumpata ikiwa West Ham itashuka daraja jambo ambalo linaonekana kuwa huenda likatokea kwa zaidi ya asilimia 70.


Marco Senesi

LIVERPOOL inajiandaa kuingia katika mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Bournemouth, Marco Senesi ili kuipata saini yake dirisha lijalo la kiangazi. Hata hivyo, taarifa zinadai Sensei ameshafanya makubaliano kwa njia ya mdomo na Tottenham ambayo ameiahidi kujiunga nayo ikiwa itasalia Ligi Kuu England. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 36 za michuano yote. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.


Curtis Jones

KIPA wa Tottenham Hotspur, Guglielmo Vicario, 29, na kiungo wa Liverpool na England, Curtis Jones, 25, wote wapo katika rada za Inter Milan dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inter inawataka ikiwa ni sehemu ya mipango ya kuboresha kikosi cha kwanza ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao na kutetea taji la Serie A ambalo imeshinda msimu huu. Mkataba wa sasa wa Curtis unatarajiwa kumalizika 2027.


Junior Kroupi

BARCELONA imevutiwa na straika wa Bournemouth, Junior Kroupi ambaye imepanga kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, lakini inatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka Manchester City na klabu nyingine Ulaya ambazo pia zimevutiwa na kiwango cha mchezaji huyo. Kroupi, 19, msimu huu amecheza mechi 32 za michuano yote na kufunga mabao 12. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2030.


Vinicius Jr

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Vinicius Jr, 25, amewaambia mabosi wa klabu hiyo anahitaji baadhi ya vitu vibadilike kabla hajafanya uamuzi wa kukubali ofa mpya. Inaelezwa mbali ya mshahara, staa huyo anataka kuhakikishiwa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na kutimiziwa  baadhi ya masharti yake. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027.


Yoane Wissa

NEWCASTLE United inadaiwa kuwa katika mpango wa kumuuza straika wa kimataifa wa DR Congo, Yoane Wissa, 29, katika dirisha lijalo la kiangazi ikiwa ni mwaka mmoja tangu imsajili. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, Newcastle inahitaji takribani Pauni 50 milioni ili kumuuza Wissa ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kusuka upya safu ya ushambuliaji. Klabu nyingi zivutiwa na staa huyo ikiwa ataweka sokoni.