Vieira amelizua huko FA baada ya kumpiga shabiki

Friday May 20 2022
Vierra PIC

LONDON, ENGLAND. KOCHA wa Crystal Palace, Patrick Vieira amempiga teke shabiki uwanjani aliyesemekana kuwa ni shabiki wa Everton baada ya mechi ya Ligi Kuu England uliyochezwa usiku wa Mei 19.

Tukio hilo limetokea baada ya mashabiki wa Everton kuingia ndani ya uwanja wa Goodison Park wakifurahia ushindi wa mabao 3-2 walioupata dhidi ya Crystal Palace na kuepekuka kushuka daraja msimu huu.

Tukio hilo la kushangaza limenaswa na video za kamera zilizopo uwanjani zikionyesha ugomvi uliyotokea kati ya Vieira na shabiki huyo wakati wakishangilia uwanjani hapo.

Chama cha soka England (FA) kinafanya uchunguzi wa sakata hilo kabla ya kutoa adhabu yoyote kwa nyota huyo wa zamani wa Arsenal.

Lakini kwa upande wa Vieira alipoulizwa kuhusu tukio hilo na waandishi wa habari aligoma kuweka wazi na kuamua kukaa kimya.

Advertisement