Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VAR yachochea vita ya ubingwa Ligi Kuu England

Muktasari:

  • Kwa sasa vita kubwa kwa ni juu ya timu mbili zinazopigania ubingwa, zile zinazowania kufuzu mashindano ya klabu Ulaya na pia zinazopambana kutoshuka daraja mwisho wa msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: MAMBO ni mengi, lakini muda mchache! Ndivyo unavyoweza kusema kuhusiana na Ligi Kuu England ambayo kimsingi imebakiza mechi mbili kumalizika, huku kukiwa na maeneo matatu yenye vita kali kwa sasa, lakini lawama kwa waamuzi nazo zimeanza kushika kasi hasa kuhusiana na penalti katika mechi zinazoendelea kutolewa nyakati hizi za lalasalama.

Kwa sasa vita kubwa kwa ni juu ya timu mbili zinazopigania ubingwa, zile zinazowania kufuzu mashindano ya klabu Ulaya na pia zinazopambana kutoshuka daraja mwisho wa msimu huu.

Kocha Pep Guardiola amefungua mashambulizi dhidi ya waamuzi baada ya “uamuzi wa VAR” ulioisaidia Arsenal kuvuna pointi tatu dhidi ya West Ham mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo anadai hajawahi kuwa na imani thabiti dhidi ya waamuzi na kwamba jambo hilo linaweza kuathiri kuhusu ubingwa.

Akizungumza kabla ya mechi ya jana dhidi ya Crystal Palace, Guardiola alisema uamuzi wa VAR ni sawa na kutupa sarafu ukiwa hewani akimaanisha kwamba kuiona inaweza bahati, huku akisisitiza kuwa City hawawezi kutegemea kile alichokiita kuwa ni msaada wa wengine kufuatia bao la West Ham lililokataliwa mwishoni mwa mchezo waliopoteza dhidi ya vinara, Arsenal.

Mtazamo wa Guardiola kuhusu waamuzi wa nchini unaongeza mkinzano kuhusu VAR katika ligi hiyo iliyoanzishwa miaka saba iliyopita, lakini aliwaambia wachezaji wake kwamba hawawezi kulaumu mtu mwingine ikiwa hawatafikia malengo yao msimu huu.

“Tulipoteza fainali mbili za FA kwa sababu waamuzi hawakufanya kazi yao ipasavyo, hata VAR,” alisema Guardiola na kuongeza:

“Wakati mambo kama haya yanatokea ni kwa sababu tunapaswa kufanya vizuri zaidi, siyo (kulaumu) waamuzi au VAR. Mimi sijawahi kuamini chochote tangu nilipofika hapa muda mrefu uliopita. Nimejifunza kila wakati kwamba unapaswa kufanya vizuri zaidi, uwe katika nafasi ya kufanya vizuri zaidi kwa sababu (VAR) ni kama kutupa sarafu ukiwa juu. VAR haikuanzishwa wikiendi iliyopita. Imekuwepo kwa miaka mingi, tumezoea, na kila mtu anajua hilo.”

Man City wanajua kuwa lazima washinde mechi zilizosalia ili kuendelea kuweka presha kwa Arsenal katika mbio za ubingwa.

Wakati Guardiola akilalamikiwa waamuzi na VAR kwa ujumla, bosi wa Chama cha Waamuzi wa Ligi Kuu England, Howard Webb alitetea uamuzi wa mwamuzi wa mechi ya Arsenal dhidi ya West Ham United akisema: “(Kulikuwa na) faulo dhidi ya kipa, bila shaka. Tumekuwa tukisema msimu mzima kwamba kama kipa anazuiwa kufanya kazi yake kwa kushikwa au kuvutwa, itakuwa penalti au faulo.”

Webb aliongeza kuwa kipa ana haki ya kulindwa kwa sababu ana uwezo wa kutumia mikono, na katika tukio hilo alizuiwa kuweza kupiga au kushika mpira, suala ambalo linapingwa na kocha wa West Ham, Nuno Espirito Santo aliyesisitiza kwamba hata waamuzi wenyewe hivi sasa wamechanganyikiwa kuhusu sheria wanazopaswa kuzisimamia.

“Wote hatuelewi ni nini ni faulo na nini si faulo. Hata waamuzi wanachanganyikiwa. Wakati mwingine kushikana kunaamriwa faulo, wakati mwingine hapana. Hakuna mwendelezo unaoeleweka. Wachezaji hawajui tena sheria,” alisema.

Nahodha wa West Ham Jarrod Bowen pia alikosoa uamuzi huo akisema VAR inachukua muda mrefu na mara nyingi inatafuta kosa hadi kulipata.

Kwa upande wa Arsenal, kocha Mikel Arteta aliunga mkono uamuzi wa VAR akisema ni sehemu ya maendeleo ya mchezo. “Ni uamuzi mgumu sana, lakini VAR imesaidia kutoa uamuzi sahihi katika mazingira yenye presha kubwa,” alisema Arteta.


MADDISON AIBUA JAMBO

Katika tukio jingine, kiungo wa Tottenham Hotspur, James Maddison amedai kuwa timu yake ilinyimwa penalti ya wazi katika mechi dhidi ya Leeds United akidai kwamba aliangushwa na Lukas Nmecha ndani ya eneo la penalti, lakini mwamuzi Jarred Gillett aliamua kuacha mchezo uendelee.

Baada ya VAR kupitia tukio hilo kwa muda mfupi, uamuzi wa awali uliendelea kubaki, lakini mchezaji huyo ameamua kulichapisha kwenye Instagram akisisitiza kuwa yeye ndiye aliyegusa mpira kwanza kabla ya kuangushwa. “Kufafanua… mguso mdogo sana wa kubadilisha mwelekeo wa mpira ulitoka nje ya mguu wangu wa kulia, si Nmecha, na nilimwambia mwamuzi hilo lakini ukaguzi (katika VAR) ulikuwa mfupi sana.”

Maddison pia aliwakosoa waamuzi kwa sasa, akisema: “Waamuzi wanaogopa kufanya uamuzi uwanjani kwa sababu ya VAR. Tunaendelea kuumizana.”

Naye Kocha wa Spurs, Roberto De Zerbi alidai presha ya uamuzi wa siku iliyotangulia (Arsenal vs West Ham) uliathiri mchezo wao na kwamba waamuzi hawakuwa watulivu, lakini akaonya juu ya mechi zijazo kwamba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa zinaenda kuamua hatima ya timu.