Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utamaduni nyota wapya NBA unavyotoweka mdogomdogo

Muktasari:

  • Kwa maana nyingine ni kuwa rookie ni mchezaji mpya kabisa kwenye NBA ama ametoka chuoni (college), ligi za nje ya Marekani au programu za maendeleo ya kikapu. Mara nyingi rookies bora hushindania tuzo ya Rookie of the Year (mchezaji bora wa kwanza mwaka huo). Mfano Victor Wembanyama anayekipiga San Antonio Spurs alikuwa rookie kwenye msimu wa 2023–2024.

KWA mashabiki wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), ambayo ndiyo maarufu zaidi kwa mchezo wa kikapu duniani watakuwa wamewahi kusikia neno 'rookies'.  Hilo linamaanisha wachezaji ambao wako kwenye msimu wao wa kwanza kucheza kwenye ligi hiyo ya kulipwa.

Kwa maana nyingine ni kuwa rookie ni mchezaji mpya kabisa kwenye NBA ama ametoka chuoni (college), ligi za nje ya Marekani au programu za maendeleo ya kikapu. Mara nyingi rookies bora hushindania tuzo ya Rookie of the Year (mchezaji bora wa kwanza mwaka huo). Mfano Victor Wembanyama anayekipiga San Antonio Spurs alikuwa rookie kwenye msimu wa 2023–2024.

Lakini, katikati ya majukumu ya rookies wa NBA kuna mabadiliko zaidi ya mila za kikapu. Awali, kubeba mabegi makubwa ya vifaa lilikuwa ni jambo la kawaida. Kuendesha gari kufuata vitafunwa supamaketi au bidhaa flani dukani ilikuwa ni sehemu ya kawaida ya kazi zao.

Vivyo hivyo kukusanya chupa tupu za maji zilizotapakaa uwanjani wakati wa mazoezi au taulo zilizoachwa sakafuni na mastaa wa timu husika kwenye chumba cha kubadilishia nguo ilikuwa suala la kawaida.

Vilevile kuwapelekea sabuni au losheni wanayopenda wachezaji wenzako wakubwa ilikuwa ni sehemu ya utamaduni kwenye orodha ya “mambo ya kufanya” ya rookie wa NBA. Wakati mwingine hata hubeba mabegi ya  kwenye safari za msimu za timu na huo waliopita mastaa wakongwe walipokuwa wakijitafuta ili kufika mbali.

Yote hayo ni sehemu ya utamaduni wa mchezo huo uliokuwepo hata kabla ya kuanzishwa kwa NBA 1946–47. Ni kama ibada inayorudiwa kila msimu kama njia ya kuwaweka sawa na kuwakaribisha wachezaji wapya kwenye vikosi.

Kwa kawaida, majukumu yao ni madogo na rahisi. Kazi zinazozalisha video za kuchekesha ambazo wachezaji au timu huposti kwenye mitandao ya kijamii, na wakati mwingine hata kuonyeshwa kwenye matangazo ya mechi za ndani zisizo za ushindani.

Kutokufuata maagizo? Hapo mambo yanaweza kuwa makali kidogo, yakikaribia aina ya unyanyasaji flani. Wachezaji wa mwaka wa kwanza waliojivuta kutekeleza majukumu hayo waliwahi kukuta nguo zao zimepotea, zimechwa au kuharibiwa na mastaa na kuna wakati hata kitanda cha hoteli kitakuwa kimelowanishwa maji.


WASIKIE HAWA

Jaylen Brown wa Boston Celtics bado anakumbuka kwa kejeli tukio ambalo wachezaji wenzake wakiongozwa na Isaiah Thomas walijaza gari lake popcorn katika msimu wake wa kwanza, kisha wakamtaka akazigawe mtaani viginevyo wasingemruhusu kufanya mazoezi akiwa nao.

Anasema alilazimika kufanya hivyo na kwamba alisaidiwa na wanafunzi katika shule kadhaa zilizokuwa jirani na nyumbani kwao waliozibeba popcorn na kwenda kuzila, huku zingine akiwapa rafiki zake.

Msimu wa 2017–18, Giannis Antetokounmpo wa Milwaukee Bucks alihisi rookie Sterling Brown hakutoa ipasavyo taulo zilizokuwa zimetapaa sakafuni, na akampa adhabu kama hiyo. Miezi minne iliyopita pia, mchezaji wa Philadelphia 76ers, Adem Bona alipatwa na tukio kama hilo ambapo tairi la gari lake lilitolewa kwa kuwa hakutimiza sharti alilopewa na wakongwe.

Draymond Green wa Golden State Warriors anasema yeye na rookies wenzake waliwahi kuachiwa bili ya chakula ya Dola 18,000 baada ya mastaa kuwakaribisha msosi hotelini kisha kutoweka.

Kocha wa Los Angeles Lakers, JJ Redick, anasimulia tukio la 2006 alipokuwa akikipiga Orlando Magic baada ya kuchelewa mazoezini, aliambiwa akae mbele ya wachezaji wenzake kuomba msamaha, lakini hali ilibadilika haraka. “Nilikuwa nimevaa kabisa (nguo za mazoezi), mara nilipokaa tu watu watatu walinishika mkono,” Redick anasema. “Walinibeba kwenye kiti wakaniweka bafuni chini ya maji baridi sana. Kila mtu aliondoka mazoezini na mhudumu wa vifaa alinitoa saa moja baadaye.”

Kinachoelezwa ni kwamba, haya yote ni maandalizi ya kumkomaza mchezaji katika timu mpya na kwamba kuna mstari mwembamba kati ya ukaribisho wa kinyenyekevu na fedheha ambao unaweza kuvukwa. Lakini habari njema kwa rookies wa NBA kwa sasa ni kwamba mambo yanaonekana kubadilika.

Wachezaji wa mwaka wa kwanza na wa pili katika All-Star Weekend mjini Los Angeles ilionyesha kwamba majukumu yao yameanza kuwa ya kawaida bila malalamiko makubwa kutoka kwao kwenda kwa mastaa na wakongwe vikosini.

All-Star Weekend ni Wikiendi ya Nyota wa NBA, ambapo huwa ni tukio la kila mwaka linalokusanya wachezaji bora wa Ligi ya Kikapu Marekani kwa ajili ya mashindano ya burudani, yakiwemo Mchezo wa Mastaa (All-Star Game), kurusha mipira ya alama tatu (3-point contest), kudanki (slam dunk contest) na rising stars (wachezaji chipukizi). Kwa kifupi ni sherehe ya vipaji na burudani katikati ya msimu wa NBA.

“Nimewahi kupewa jukumu la kuwaletea Chick-fil-A wachezaji, lakini si zaidi ya hapo,” anasema Tre Johnson wa Washington Wizards.

Chick-fil-A ni mnyororo wa migahawa ya vyakula vya haraka (fast food) huko Marekani unaojulikana kwa vyakula vinavyotokana na kuku, hasa mikate ya nyama ya kuku wa kukaanga.

Staa wa Miami Heat, Kel'el Ware anasema utamaduni wa timu yake haukumlazimisha kubeba mizigo ya mtu, badala yake alikuwa huru kujichanganya na nyota wa kikosi hicho katika mambo mbalimbali ikiwamo mitoko binafsi na starehe za mitaani. Hivyo ndivyo pia ilivyokuwa kwa Stephon Castle wa San Antonio Spurs ambaye alikuwa Rookie wa 2025 katika kikosi chake.

Upande mwingine wa rookie ni kutumwa kutekeleza kazi ndogo ndogo, lakini wakiwekwa chini ya wakongwe wanaowalea ikiwa ni katika kuwawezesha kuchota hekima, mbinu na uzoefu, na katika hilo wachezaji kadhaa vijana  wamefaidika na hilo.

“Nilimtegemea sana Khris,” anasema Alex Sarr wa Washington Wizards akimzungumzia Khris Middleton ambaye alihamia Dallas Mavericks. “Labda Chris Paul, huyu alikuwa bora kwangu na alikuwa kama kocha kwa wote,” anaongeza Castle akizungumzia kipengele hicho.

Kuna pia utamaduni wa 'kulipa fadhila' upande huu wa uhusiano wa rookie na wakongwe, na kwa mfano, Jaylen Wells wa Memphis Grizzlies sasa anajaribu kuwasaidia Cedric Coward na Javon Small kama alivyosaidiwa na Marcus Smart na Jaren Jackson Jr.

Charlotte Hornets pia wana kundi kubwa la rookies wakiwamo Kon Knueppel, Ryan Kalkbrenner, Sion James na Liam McNeeley ambao wameonyesha unyenyekevu kulingana na Grant Williams.

Williams pamoja na Pat Connaughton na Mason Plumlee, hivi sasa ni mastaa wakongwe ndani ya chumba cha kubadilishia nguo ingawa hawajasahau walikotoka.

“Nimefundishwa hivyo,” anasema Williams akiwataja Kemba Walker (sasa kocha wa Charlotte), Al Horford na Daniel Theis ambao walimtunza mwaka wake akiwa rookie, akikumbuka tukio la chakula Miami alipolazimika kununua chupa ya mvinyo ya Dola 2,000 akidhani atailipia, lakini Theis akamzuia.

“Sasa mimi ndiye ninalipa,” anasema Williams, “na natumaini hawa rookies wataendeleza utamaduni huo kwa kizazi kijacho.”