Uholanzi yatangulia robo fainali Kombe la Dunia

Uholanzi imeandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia 2022, Qatar kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Marekani mabao 3-1.
Marekani imekubali kichapo hicho katika Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa na rasmi itaaga mashindano hayo huku Uholanzi ikisubiri mshindi kati ya Argentina dhidi ya Australia.
Argentina na Australia zitamenyana leo majira ya saa 4:00 usiku.
Hii inakuwa mara sita kwa taifa hili kufuzu kucheza robo fainali mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1974 ambapo ilifika hadi fainali na kuopoteza mbele ya Ujerumani ya Magharibi,
Historia inaonyesha kuwa ni mara moja tu ndio wababe hawa walishindwa kuendelea mbele baada ya kufika robo fainali ambayo ilikuwa ni mwaka 1994 ambapo walipoteza mbele ya Brazil ambapo ilipoteza kwa mabao 3-2.
Uholanzi imerejea baada ya kushindwa kufuzu michuano ya mwaka 2018 iliyofanyika kule nchini Urusi ambapo ilishindwa kufuzu.