Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tudor akataa kuthibitisha hatma yake Tottenham baada ya vipigo vitatu

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Croatia amepoteza mechi zote tatu tangu alipochukua nafasi ya kuinoa Spurs, huku timu hiyo ikiwa kwenye hatari kubwa ya kushuka daraja.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Tottenham Hotspur, Igor Tudor, ambaye yuko kwenye presha kubwa, amekataa kuthibitisha kama bado atakuwa kocha wa timu hiyo katika mechi ijayo.

Kocha huyo raia wa Croatia amepoteza mechi zote tatu tangu alipochukua nafasi ya kuinoa Spurs, huku timu hiyo ikiwa kwenye hatari kubwa ya kushuka daraja.

Kipigo cha 3-1 nyumbani dhidi ya Crystal Palace, Alhamisi kimeiacha Spurs ikiwa pointi moja tu juu ya eneo la kushuka daraja, huku mechi tisa zikiwa zimebaki kumaliza msimu.

Baada ya mechi, Tudor alionekana kuwa na hasira. Alipoulizwa kama atakuwa kwenye benchi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid, Jumanne, kocha huyo wa zamani wa Juventus alitoa jibu la maneno mawili: “Sina majibu.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 pia alikataa kujibu maswali mengine kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo, aliposema: “Sifikirii kuhusu jambo hilo. Nina kazi ya kufanya, hiyo tu.”

Tudor bado ana matumaini ya kuokoa Spurs. Licha ya kipigo hicho na Spurs ilikuwa imeanza kwa kuongoza kabla ya kuporomoka katika kipindi cha kwanza, Tudor alisema ana imani zaidi kuhusu timu yake kuepuka kushuka daraja.

Alisema: “Inaweza kusikika ajabu, lakini baada ya mchezo huu ninaamini zaidi kuliko nilivyoamini kabla. Nimeona kitu fulani, nguvu, ari na mapambano. Nahitaji kuchagua wachezaji sahihi kwa sababu boti inaelekea upande ninaotaka iende. Wale waliomo kwenye boti wanaweza kubaki, wengine wanaweza kuondoka.” Mechi ijayo kwenye Ligi Kuu England, Spurs itakuwa ugenini kukipiga na Liverpool, Machi 15.