Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuchel abariki mastaa England kuzomewa

TUCHEL Pict

Muktasari:

  • Harry Kane alifunga bao la ushindi kipindi cha pili, lakini hiyo haikubadilisha chochote kwa mashabiki wa England walioonekana kuwazomea wachezaji wao, huku pia wakiimba nyimbo za kumsema Waziri mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel aliwakosoa vikali wachezaji wake kwa ‘kuchezea moto’ katika ushindi mwembamba kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Andorra usiku wa Jumamosi, walibahatika kidogo tu, lasivyo wangetoka sare au kufungwa.

Harry Kane alifunga bao la ushindi kipindi cha pili, lakini hiyo haikubadilisha chochote kwa mashabiki wa England walioonekana kuwazomea wachezaji wao, huku pia wakiimba nyimbo za kumsema Waziri mkuu wa nchi hiyo Keir Starmer.

Ingawa Tuchel alisema hakuweza kusikia nyimbo hizo dhidi ya Starmer, alikiri hawezi kuwalaumu mashabiki kwa kuzomea kikosi chake.

"Nadhani mwishowe tulichezea moto, kwa kweli," alisema Tuchel. "Nguvu ziliisha wakati ambao tulihitaji kuzitumia zaidi. Lakini tuliibuka na ushindi. Nafikiri bado tuliustahili ushindi huo na sasa tuna ushindi wa tatu mfululizo na hatujaruhusu bao lolote."

"Sikupenda jinsi tulivyomaliza mchezo. Nilipenda tulivyoanza, dakika 25 za mwanzo, lakini dakika 25 za mwisho sikuzipenda. Nafikiri tulikosa umakini na uharaka unaohitajika kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia. Tulichezea moto. Sikupenda uchezaji wa wachezaji wangu mwisho wa mechi. Lugha ya miili yao haikuendana na umuhimu wa tukio hilo."

England watakabiliana na Senegal katika mechi ya kirafiki kwenye uwanja wa City Ground wa Nottingham Forest Jumanne ijayo na Tuchel aliongeza: “Zomeazomea ni sawa. Kwanza kabisa, sapoti yao katika mechi ilikuwa ya ajabu, ilitengeneza mazingira ya kuvutia kwa mechi kama hii. Nilipotoka nje, nilihisi msisimko.

"Walivunjika moyo na hawakufurahishwa na kiwango chetu, hasa jinsi tulivyomaliza kipindi cha kwanza. Sidhani kama tunaweza kuwalaumu kwa hilo.”

Kuhusu nyimbo dhidi ya Starmer, aliongeza: “Sikusikia lolote kuhusu nyimbo za matusi au matusi ya wazi. Kama ilitokea, bila shaka haikubaliki, lakini mimi sikuyasikia.”