Terry amuaga Marina, Bruce

Terry amuaga Marina, Bruce

LONDON, ENGLAND. BEKI wa zamani wa Chelsea, John Terry  amemuaga aliyekuwa Murugenzi msaidizi wa klabu hiyo Marina Granovskaia baada ya kuachia ngazi.
Marina aliachia ngazi sambamba na Bruce Buck aliyekuwa mwenyekiti wa The Blues tangu mwaka 2003.
Terry alimshukuru Marina kwa mchango wake kwa maendeleo na mafanikio aliyoleta ndani ya klabu hiyo chini ya uongozi wake.
Beki huyo kisiki aliandika ujumbe mrefu kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye maneno ya shukrani kwao.
“Nawashakuru kwa kazi kubwa waliyofanya, walinipa sapoti kubwa sana ndani na je ya uwanja, kwa pamoja mmeijenga timu upande wa wanawake na wanaume, vile vile namtakia kila kheri mmiliki wetu mpya Todd  Boehly, kumbukumbu ya Marina na Bruce itabakia milele,” aliandika Terry.