Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag kapiga Euro 100,000 kwa siku

TEN Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo Mdachi, Ten Hag alifutwa kazi Leverkusen baada ya kuiongoza timu hiyo kwenye mechi tatu tu za kiushindani, huku mechi mbili zikiwa ni za Bundesliga.

MUNICH, UJERUMANI: KOCHA, Erik ten Hag ameigharimu Bayer Leverkusen mkwanja mrefu, Euro 100,000 kwa kila siku aliyokuwa akifanya kazi katika klabu hiyo ya Bundesliga, imeelezwa.

Kocha huyo Mdachi, Ten Hag alifutwa kazi Leverkusen baada ya kuiongoza timu hiyo kwenye mechi tatu tu za kiushindani, huku mechi mbili zikiwa ni za Bundesliga.

Ten Hag alitua Leverkusen kurithi mikoba ya Xabi Alonso. Leverkusen iliuza mastaa wake kadhaa ambao waliipa timu hiyo mataji mawili msimu wa 2023-24 akiwamo Florian Wirtz na Granit Xhaka, jambo lililomfanya kocha mpya kwenye timu hiyo kuwa na kazi ya kukijenga kikosi upya

Lakini, alipewa siku 60 kwenye kibarua hicho kabla ya mabosi wa Leverkusen kuamua kumfungulia mlango wa kutokea baada ya kupoteza uongozi wa mabao 3-1 na kuambulia sare ya 3-3 dhidi ya Werder Bremen iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani.

Hilo lilimfanya Ten Hag awe ameambulia pointi moja tu kwenye Bundesliga baada ya mechi mbili, huku akiwa ameshuhudia ushindi wa 4-0 kwenye mechi ya kombe dhidi ya timu ya daraja la nne, Sonnenhof Grossaspach.

Kwa mujibu wa Bild, Ten Hag atalipwa fidia ya Euro 6 milioni baada ya Leverkusen kuona ni heri kumfuta kazi kocha huyo sasa kuliko kuendelea kusubiri.

Hata kabla ya Ten Hag kufutwa kazi, Bild liliripoti kwamba klabu hiyo ilikuwa ikifanya usajili wa wachezaji wapya bila ya kumweleza kocha wao.

Beki wa zamani wa Real Madrid, Lucas Vazquez alijiunga bure na timu hiyo baada ya kufanya mawasiliano na mkurugenzi wa michezo, Simon Rolfes, huko kocha Ten Hag akidai kwamba alikutana na mchezaji huyo wakati tayari akiwa ameshafanyiwa vipimo vya afya na kusaini mkataba.

Lakini, kwa fidia hiyo ya Euro 6 milioni na siku ambazo Ten Hag aliongoza Leverkusen hiyo ina maana aliigharimu timu hiyo Euro 100,000 kwa siku.