Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Suarez hatihati kwenda Kombe la Dunia 2026

SUAREZ Pict
SUAREZ Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vimeripoti kuwa kocha wa timu hiyo ya taifa Marcelo Bielsa ameamua kutomjuisha mshambuliaji huyo wa Inter Miami ya Marekani katika kikosi chake cha wachezaji 55 wa kwanza alichokikabidhi kwa FIFA.

Ndoto ya mshambuliaji Luis Suarez kucheza kwa mara ya tano Kombe la Dunia akiwa na Uruguay ipo shakani. 

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vimeripoti kuwa kocha wa timu hiyo ya taifa Marcelo Bielsa ameamua kutomjuisha mshambuliaji huyo wa Inter Miami ya Marekani katika kikosi chake cha wachezaji 55 wa kwanza alichokikabidhi kwa FIFA.

SUAR 01

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, vimedai kuwa kocha huyo wa Uruguay amemuacha Suarez mwenye miaka 39 katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 55 alichokipeleka FIFA.

Ni uamuzi mzito utakaozima ndoto ya Suarez kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya tano.

SUAR 02



Kocha Bielsa, ameweka wazi imani yake kubwa ipo kwa wachezaji vijana atakaowatumia katika fainali zitakazofanyika Marekani, Canada, na Mexico. 

Suarez anabaki kuwa mmoja wa wachezaji wenye historia kubwa katika soka la Uruguay akiwa kinara wa ufungaji wa muda wote wa taifa hilo kwa kufunga mabao 69 katika mechi 143 alizocheza na taifa hilo.