Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sterling pasua kichwa Chelsea

Muktasari:

  • Lakini, Chelsea na Sterling watahitaji zaidi kupata dili la kuondoka jumla, huku vita kali ikibaki kwenye mapambano ya kukwepa kile kilichotokea kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, wakati winga huyo Mwingereza aliponaswa na Arsenal katika dakika za mwisho kabisa kabla dirisha kufungwa.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA imepanga kumtoa tena kwa mkopo Raheem Sterling huku ikipambana kuwapiga bei mastaa 10 kabla ya dirisha la usajli kufungwa.

Lakini, Chelsea na Sterling watahitaji zaidi kupata dili la kuondoka jumla, huku vita kali ikibaki kwenye mapambano ya kukwepa kile kilichotokea kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, wakati winga huyo Mwingereza aliponaswa na Arsenal katika dakika za mwisho kabisa kabla dirisha kufungwa.

Chelsea inapambana kuwapiga bei Sterling, Nicolas Jackson, Christopher Nkunku, Axel Disasi, Renato Veiga, Carney Chukwuemeka, David Datro Fofana na Ben Chilwell ndani ya siku chache. Kinda winga Tyrique George naye ataelekea mlango wa kutokea, wakati beki Aaron Anselmino naye anaonekana kama mchezaji wa ziada kwenye kikosi hicho cha kocha Enzo Maresca.

Sterling mkataba wake umebakiza miaka miwili, huku akilipwa Pauni 300,000 kwa wiki. Msimu uliopita, Chelsea ilikuwa ikilipa sehemu ya mshahara huo wakati alipokuwa akicheza kwa mkopo huko Arsenal.

Sterling atapenda kubaki England tena London, ambako mwanaye, Thiago, 8, amejiunga kwenye akademie ya Arsenal mapema katika dirisha hili la kiangazi. Fulham ilionyesha dhamira ya kuhitaji saini yake.