Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa S’oton amuopa mtoto wa Roy Keane

Muktasari:

  • Sherehe hiyo ilifanyika katika Kin House, jumba la kihistoria lililokarabatiwa na kutumika kwa hafla maalumu za watu binafsi, ambapo familia, marafiki na wageni mbalimbali kutoka ulimwengu wa soka walihudhuria tukio hilo.

LONDON,  England: LEAH Keane ambaye ni binti wa nguli wa zamani wa Manchester United, Roy Keane, amefunga ndoa na beki wa Southampton, Taylor Harwood-Bellis, katika harusi ya kifahari huko Wiltshire, Uingereza.

Sherehe hiyo ilifanyika katika Kin House, jumba la kihistoria lililokarabatiwa na kutumika kwa hafla maalumu za watu binafsi, ambapo familia, marafiki na wageni mbalimbali kutoka ulimwengu wa soka walihudhuria tukio hilo.

Inaeleweka kwamba Leah ndiye binti kipenzi cha Keane ambaye amekuwa akitembea naye katika sehemu mbalimbali licha ya kuwa na umri mkubwa.

Moja ya matukio yaliyovutia hisia nyingi wakati wa harusi hiyo ilikuwa Roy Keane kumtembeza binti yake kwenda madhabahuni, jambo lililoonyesha upande wa kifamilia wa nyota huyo anayejulikana kwa ukali wake akiwa mchezaji na mchambuzi wa soka.

Harwood-Bellis, mwenye umri wa miaka 24, alimposa Leah 2024 wakati wa mapumziko nchini Italia, na wawili hao tayari wana mtoto mmoja wa kike aitwaye Iris ambaye alizaliwa Desemba, mwaka jana. Miongoni mwa wageni waliokuwepo alikuwa mchezaji mwenzake Harwood-Bellis wa Southampton, Jack Stephens.

Harwood-Bellis amewahi kusema kuwa Roy Keane ni mmoja wa watu wanaompa ushauri muhimu katika maisha ya soka, akieleza kuwa daima amekuwa akimtakia mema na kumsaidia kufanya uamuzi sahihi.

Kwa upande wake, Keane pia amewahi kumpongeza mkwe wake mpya akimtaja kuwa kijana mwenye tabia nzuri na aliyepata malezi bora kutoka kwa familia yake. Harusi hiyo imefanyika muda mfupi baada ya Harwood-Bellis kupitia kipindi kigumu akiwa Southampton, lakini sasa ameanza sura mpya ya maisha yake binafsi baada ya kufunga ndoa na Leah.