Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taharuki! Sanamu za wachezaji zaporomoshwa Mexico

Muktasari:

  • Kundi hilo la walimu, linalohusishwa na chama cha CNTE, lilivamia eneo lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya maonyesho ya mashindano ya Kombe la Dunia, likivunja sanamu kubwa za wachezaji, kuzivua jezi na baadaye kuzichoma moto pamoja na mipira.

MEXICO CITY,   MEXICO: MJI wa Mexico City upo kwenye taharuki baada ya kundi la walimu wanaogoma kufanya maandamano yaliyohusisha kuharibu na kuchoma moto sanamu za wachezaji wa mpira zilizokuwa sehemu ya maonyesho ya Kombe la Dunia 2026.

Kundi hilo la walimu, linalohusishwa na chama cha CNTE, lilivamia eneo lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya maonyesho ya mashindano ya Kombe la Dunia, likivunja sanamu kubwa za wachezaji, kuzivua jezi na baadaye kuzichoma moto pamoja na mipira.

Walimu hao walikuwa wakipinga masuala ya mishahara na mageuzi ya pensheni, wakisisitiza kuwa hawatakubali hali ya sasa iendelea na wakitishia kuendelea na maandamano hadi suluhisho lipatikane, huku baadhi yao wakionekana kufunga barabara kuu katika mji huo mkuu.

Kaulimbiu ya baadhi ya waandamanaji ilikuwa ikisema: “Kama hakuna suluhisho, mpira hautachezwa,”  ikionyesha nia yao ya kuvuruga maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya soka.

Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, alilazimika kubadili mkutano wake wa ana kwa ana na badala yake kufanya kupitia mtandao kutokana na waandamanaji kuziba lango la Ikulu ya Taifa.

Siku moja kabla ya tukio hilo, maandamano mengine yaliripotiwa ambapo polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakielekea katika Uwanja wa Zocalo.