Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot akijipindua tu hana chake

Muktasari:

  • Usiku wa Jumatano, miamba hiyo ya Anfield ilikuwa na kasheshe la kuwakabili wababe wa Ujerumani, Eintracht Frankfurt kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabaingwa Ulaya, kilichotokea kimetokea.

LIVERPOOL, ENGLAND: LISEMWALO ni kwamba kibarua cha Arne Slot huko Liverpool kipo kwenye mashaka makubwa kutokana na timu hiyo kupata matokeo ya hovyo uwanjani.

Usiku wa Jumatano, miamba hiyo ya Anfield ilikuwa na kasheshe la kuwakabili wababe wa Ujerumani, Eintracht Frankfurt kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabaingwa Ulaya, kilichotokea kimetokea.

Lakini, kipigo ilichokipata kutoka kwa mahasimu wao Manchester United kwenye Ligi Kuu England kiliwafanya kushuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo, wakati kuna kipindi ilikuwa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.

Kipigo hicho ilichokumbana nacho Anfield kilikuwa cha nne mfululizo, hivyo usiku wa Jumatano ilikuwa inapambana kukwepa kipigo cha tano mfululizo. Jambo hilo limedaiwa kumweka kwenye kitimoto kocha Slot, wakati Liverpool ikiwa imecheza mechi nane tu.

Kwa mujibu wa Fichajes, vipigo hivyo vinne ilivyokumbana navyo Liverpool vimeiweka ajira ya kocha Slot kwenye matatizo makubwa. Mabosi wa Anfield wanadaiwa kuanza kutia shaka juu ya uwezo wake katika kuifikisha juu zaidi klabu hiyo. Bodi ya wakurugenzi wa Liverpool wanataka kocha mwenye uwezo wa kuituliza timu yake na kupambania mataji.