Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri ya dili la Gyokeres Arsenal

Muktasari:

  • Staa huyo amekamilisha uhamisho wake wa Pauni 63.7 milioni na amesaini dili refu la kukipiga Emirates akiwa anatokea Sporting CP ya Ureno.

LONDON, ENGLAND: STRAIKA, Viktor Gyokeres amefunguka anadhani Arsenal ni klabu mwafaka kwake kuwa hapo na kuwaahidi kuwapa mashabiki wa timu hiyo kitu cha kushangilia msimu huu.

Staa huyo amekamilisha uhamisho wake wa Pauni 63.7 milioni na amesaini dili refu la kukipiga Emirates akiwa anatokea Sporting CP ya Ureno.

Gyokeres, 27, alikuwa mmoja wa wachezaji waliozungumzwa sana dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya kuhusishwa na klabu kibao.

Arsenal imemnasa na hivyo kuamua kuachana na mpango wa kumchukua straika wa RB Leipzig, Benjamin Sesko.

Na kinachoonekana, Gyokeres hakuhitaji kushawishiwa sana ili kumwaga wino wa kuichezea Arsenal.

Gyokeres, aliyefunga mabao 54 msimu uliopita, ameorodhesha sababu tano ambacho hakika zimemshawishi kwenda kujiunga na Arsenal.

“Nilihisi hii ni klabu mwafaka kwangu,” alisema baada ya kusaini.

“Nilichokiona kwa miaka iliyopita na namna wanavyocheza soka lao. Nilipocheza dhidi yao, niligundua ni timu ngumu kukabiliana nao.

“Hilo limenifanya niichague Arsenal na kingine ni historia yao pamoja na mashabiki. Inavutia kwa sapoti ambayo mashabiki wamenipa kabla hata sijaja. Hilo ni jambo kubwa. Itakwenda kuwa vizuri zaidi tukikutana uwanjani.”