Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku ya hukumu, Droo hatua ya 16 UEFA kufanyika leo

Muktasari:

  • Droo hiyo ambayo itachezeshwa kuanzia saa 8:00 mchana kwa saa za hapa Tanzania, itahusisha jumla ya timu 16 ambazo baadhi zilifanikiwa kupita baada ya mechi za mchujo juzi na jana.

NYON, USWISI: MACHO na masikio yote leo yanageuzwa kule kwa jijini Nyon, Uswisi ambako droo ya hatua ya 16 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa inachezeshwa.

Droo hiyo ambayo itachezeshwa kuanzia saa 8:00 mchana kwa saa za hapa Tanzania, itahusisha jumla ya timu 16 ambazo baadhi zilifanikiwa kupita baada ya mechi za mchujo juzi na jana.

Katika timu hizo 16, nane za kwanza ni zile zilizofuzu moja kwa moja hatua hiyo baada ya kushika nafasi nane za juu ambazo ni pamoja na vinara Arsenal, Bayern Munchen, Liverpool, Tottenham, Barcelona, Chelsea, Sporting CP na Manchester City.

Timu nane nyingine zinazokamilisha 16-Bora, ni zile ambazo zilipita baada ya kucheza mechi za mtoano ambazo ni pamoja na Real Madrid, PSG, Newcastle, Atletico Madrid, Atalanta, Bayer Leverkusen, Galatasaray na  Bodo/Glimt.

Kwa mujibu wa muundo wa droo hiyo, kila timu tayari imebakiza wapinzani wawili tu inaoweza kukutana nao katika hatua ya mchujo.

Baada ya kumaliza kileleni kwenye msimamo wa ligi, Arsenal inatarajiwa kukutana na aidha Atalanta au Bayer Leverkusen, ambayo ilipita hatua ya mtoano baada kuitoa  Borussia Dortmund wakati Atalanta ikiitoa Olympiacos.

Kwa upande mwingine, timu nyingine za England zinakabiliwa na changamoto kubwa zaidi. Baada ya kupita kwa urahisi dhidi ya Qarabag, Newcastle itapangwa aidha dhidi ya Chelsea au Barcelona katika hatua ya 16 bora.

Chelsea kama haitakutana na Newcastle, basi itakutana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Paris Saint-Germain.

Endapo droo itaamua matokeo tofauti, kuna uwezekano mkubwa PSG ikakutana na Barcelona katika hatua ya robo fainali.

Wakati huohuo, Tottenham Hotspur na Liverpool zote zitakutana na aidha Atletico Madrid au Galatasaray katika hatua hiyo.

Manchester City pia huenda ikaumana na aidha Bodo/Glimt au vigogo Real Madrid, pia Sporting Lisbon huenda ikaumana na Real Madrid au Bodo/Glimt.

Mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Machi 10–11, huku zile za marudiano zikipigwa wiki moja baadaye baada ya zile za mkondo wa kwanza.

Katika robo fainali, timu itakayocheza dhidi ya PSG ambazo ni aidha Barcelona au Chelsea zitakutana na aidha Liverpool, Galatasaray au Tottenham ikiwa zitashinda mechi zao za mtoano.

Endapo Madrid itapita huenda ikakutana na Atalanta, Arsenal au Bayern Munich.

Vilevile Newcastle ikiwa itapata ushindi katika mechi yake ya 16-Bora ambayo inaweza kucheza dhidi ya Chelsea au Barcelona itakutana na Atletico, Tottenham au Liverpool.

Upande mwingine ikiwa Borussia Dortmund itashinda mechi yake ya 16-Bora ambapo inaweza kukutana na Man City au Sporting Lisbon, inaweza kukutana na Leverkusen, Bayern Munich au Arsenal.


HATUA NYINGINE

ROBO FAINALI: Aprili 7/8 kwa mechi za mkondo wa kwanza na Aprili 14/15 kwa mkondo wa pili.

NUSU FAINALI: Aprili 28/29 kwa mkondo wa kwanza na Mei 5/6 kwa mkondo wa pili.

FAINALI: Itakuwa Mei 30,2026 huko Budapest, Hungury.