Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shearer: Isak? Kule kuna yule Ekitike

ISAK Pict

Muktasari:

  • Liverpool ilianza msimu wa Ligi Kuu England kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bournemouth usiku wa Ijumaa, huku straika Ekitike alikuwa staa wa mchezo.

NEWCASTLE, ENGLAND: GWIJI Alan Shearer amemuonya Alexander Isak kwamba hatakuwa na uhakika wa kuanzishwa huko Liverpool baada ya Hugo Ekitike kuanza vyema kabisa maisha yake kwenye kikosi hicho cha Anfield.

Liverpool ilianza msimu wa Ligi Kuu England kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Bournemouth usiku wa Ijumaa, huku straika Ekitike alikuwa staa wa mchezo.

Straika huyo Mfaransa, ambaye amenaswa na Liverpool kwa ada ya Pauni 79 milioni, ambapo Pauni 69 milioni za utangulizi na Pauni 10 milioni zitalipwa kama bonasi huko kwenye klabu yake ya Eintracht Frankfurt.

Ekitike alifunga bao la kuongoza kabla ya mapumziko na kisha akaasisti la Cody Gakpo kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-0. Bournemouth ilipambana na kufunga mara mbili kupitia kwa Antoine Semenyo, lakini Federico Chiesa na Mohamed Salah waliongeza mabao mengine kwa upande wa Liverpool na kuanza msimu huu wa Ligi Kuu England kwa kukusanya pointi tatu.

Wakati kukiwa na wasiwasi juu ya beki ya Liverpool, straika Ekitike alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi.

“Ni wazi, mshambuliaji yeyote anayefikiria kwenda Liverpool, atapaswa kufikiria upya kutokana na ule ubora wa Ekitike,† aliandika Shearer kwenye X.

Liverpool ilipeleka ofa ya Pauni 110 milioni pamoja na bonasi ya Pauni 10 milioni kwa ajili ya Isak, lakini Newcastle ikataa.Liverpool imewapiga bei washambuliaji Darwin Nunez na Luis Diaz kwenye dirisha hili na imempoteza fowadi wake, Diogo Jota, aliyefariki dunia ajalini.