Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sesko akili yote Man United

Muktasari:

  • Taarifa kutoka tovuti ya The Athletic zinabainisha Sesko amewaarifu RB Leipzig na mawakala wake chaguo lake ni Man United. Newcastle ilikuwa tayari imefikia makubaliano na Leipzig kwa ofa ya Pauni  78  milioni, lakini mchezaji huyo amekataa kujiunga nao.

MANCHESTER, ENGLAND: MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Slovenia, Benjamin Sesko, 22, inadaiwa amekubali kujiunga na Manchester United na kuikataa Newcastle United iliyokuwa inahitaji huduma yake pia.

Taarifa kutoka tovuti ya The Athletic zinabainisha Sesko amewaarifu RB Leipzig na mawakala wake chaguo lake ni Man United. Newcastle ilikuwa tayari imefikia makubaliano na Leipzig kwa ofa ya Pauni  78  milioni, lakini mchezaji huyo amekataa kujiunga nao.

Hii inakuwa ni mara nyingine Newcastle kukataliwa dirisha hili baada ya kutokea hivyo kwa James Trafford, Hugo Ekitike, Joao Pedro, Matheus Cunha na Bryan Mbeumo  ambao wote walichagua klabu nyingine.

Sesko alikuwa pia akihusishwa na Arsenal, lakini washika mitutu hao  waliamua kumsajili Viktor Gyokeres badala yake.

Man United imeripotiwa imewasilisha ofa ya Pauni 73.8 milioni, ambayo bado inajadiliwa lakini jambo linalowapa faida ni mchezaji mwenyewe kuwa tayari kujiunga nao.

Masuala ya masilahi binafsi hayatarajiwi kuwa tatizo, kwani Man United inataka kumpa karibia mara tatu ya mshahara wake wa sasa.

Ikiwa dili hili litakamilika, linaweza kuashiria mwisho wa safari ya Rasmus Hojlund katika viunga vya Old Trafford.

Hojlund amewekwa sokoni na anauzwa kwa Pauni 30 milioni na inaelezwa anatarajiwa kuondoka ili kumpisha Sesko anayetarajiwa kuwa sehemu ya safu mpya ya ushambuliaji ya Man United ambayo tayari ina Matheus Cunha na Bryan Mbeumo.

Kwa upande wa Newcastle, hali inazidi kuwa ngumu hasa baada ya mshambuliaji wao Alexander Isak kuonyesha nia ya kuondoka. Liverpool tayari iliwasilisha ofa ya Pauni 120 milioni iliyokataliwa na sasa wanaandaa ofa nyingine.

Isak, kama ilivyo kwa Sesko, amekuwa akifanya mazoezi peke yake, jambo linalozidisha tetesi za uhamisho wake dirisha hili.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, amekiri hadharani dirisha hili la usajili limekuwa gumu kwao: "Tumekosa wachezaji wengi tuliohitaji kwa sababu mbalimbali. Lakini bado tuko sokoni na tutaendelea kupambana hadi dirisha la usajili litakapofungwa. Tunataka wachezaji bora tu na tunatanguliza ubora kuliko idadi. Hiyo ndiyo njia pekee ya kufika tunapotaka kufika."