Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Semenyo aichagua Liverpool, vigogo wengine bado wanamtaka

Muktasari:

  • Semenyo amekuwa akiwindwa na vigogo wengi barani Ulaya tangu dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha akiwa na Bournemouth.

LIVERPOOL inatajwa kuwa ndio timu iliyochaguliwa na mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo licha ya klabu nyingine za Ligi Kuu England zikiwemo Tottenham, Arsenal na Manchester City kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Semenyo amekuwa akiwindwa na vigogo wengi barani Ulaya tangu dirisha lililopita la usajili wa majira ya kiangazi kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha akiwa na Bournemouth.

Mkataba wa sasa wa Semenyo na Bournemouth unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Tangu kuanza kwa msimu huu, mshambuliaji huyo amecheza mechi 16 za michuano yote na kufunga mabao matano.

Semenyo amekuwa akihitajika na Liverpool tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi na inaonekana staa huyu amevutiwa sana na mipango yao.

Liverpool inataka kuhakikisha inamsajili Januari mwakani ili akazibe pengo la Mohamed Salah ambaye atakuwa anaitumikia Misri katika michuano ya AFCON kwa wakati huo.


Marc Guehi

BEKI wa Crystal Palace, Marc Guehi ameendelea kuwa katika rada za Liverpool kuelekea dirisha lijalo la usajili la majira ya baridi. Mbali ya Liverpool iliyokuwa karibu kuipata saini yake katika dirieha lililopita, Barcelona pia inahitaji huduma yake, lakini inataka kusubiri hadi mwisho wa msimu ambapo mkataba wake unatarajiwa kumalizika. Guehi ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na klabu nyingi barani Ulaya, kutokana na kiwango chake alichoonyesha msimu uliopita akiwa na Palace pamoja na hali yake ya mkataba.


Joshua Zirkzee

ROMA imeanza mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Joshua Zirkzee, katika dirisha la usajili la Januari. Ili kufanikisha dili hilo, Roma imepanga kwanza kuachana na straika wa Brighton na timu ya taifa ya Ireland, Evan Ferguson ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika kikosi chao. Zirkzee amekuwa akihusishwa na mipango ya kuondoka Manchester United kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha mashetani wekundu hao.


Jack Grealish

KIUNGO wa Manchester City anayecheza kwa mkopo wa msimu mmoja Everton, Jack Grealish, 30, amefunguka kwamba anajisikia furaha katika kikosi hicho na anatamani kuendelea kusalia klabuni hapo kwa kusaini mkataba wa kuendelea kudumu. Inaelezwa Grealish anaamini akiendelea kucheza katika kikosi cha Everton atakuwa na nafasi kubwa ya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Niclas Fullkrug

WEST  Ham ipo tayari kumuuza mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ujerumani,  Niclas Fullkrug mwenye umri wa miaka 32. Staa huyu anaripotiwa kuwa katika rada za AC Milan inayohitaji kumsajili kwa mkopo wa nusu msimu katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Milan inataka kumsajili staa huyu kwa mkopo kwa sababu haina bajeti ya kumnunua jumla, lakini itamsainisha mkataba wa kudumu mwisho wa msimu endapo itaridhishwa na kiwango chake.


Luis Suarez

INTER MIAMI ipo katika hatua za mwisho za kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa mwezi huu. Mkataba huo mpya unatarajiwa kumweka Suarez katika kikosi cha Miami hadi mwaka 2026. Suarez amekuwa na mchango mkubwa tangu ajiunge na Inter Miami, hali iliyowashawishi viongozi wa klabu hiyo kuendelea kumwamini licha ya umri kumtupa mkono.


Davide Bartesaghi

ARSENAL inmafuatilia kwa karibu beki wa pembeni wa AC Milan, Davide Bartesaghi, mwenye umri wa miaka 19 ambaye inataka kumsajili kama sehemu ya mipango ya kuimarisha safu ya ulinzi. Bartesaghi bado ana mkataba wa muda mrefu hadi na Milan hadi mwaka 2030, hivyo timu hiyo inadaiwa kutaka kiasi kikubwa cha pesa ili kumuuza kinachokadiriwa kufikia Pauni 45 milioni.


Youri Tielemans

ASTON VILLA inapanga kuanza mazungumzo na kiungo wao wa kimataifa wa Ubelgiji,  Youri Tielemans kuhusu kumsainisha mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho. Mkataba wa sasa wa Tielemans unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, lakini Villa inataka kumsainisha mkataba mpya mapema baada ya kuona baadhi ya vigogo barani Ulaya wameanza harakati za kumnyemelea.