Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sancho kufanywa chambo kwa Baleba

SANCHO Pict

Muktasari:

  • Man United inamtazama Baleba kama mchezaji wao muhimu wa kumnasa dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini Brighton inamthaminisha staa huyo wa Cameroon kuwa na thamani inayozidi Pauni 100 milioni.

LONDON, ENGLAND: WINGA Jadon Sancho huenda akatumika kama sehemu ya ofa ya Manchester United katika mchakato wao wa kuwashawishi Brighton ili kumnasa kiungo wa boli, Carlos Baleba.

Man United inamtazama Baleba kama mchezaji wao muhimu wa kumnasa dirisha hili la majira ya kiangazi, lakini Brighton inamthaminisha staa huyo wa Cameroon kuwa na thamani inayozidi Pauni 100 milioni.

Ripoti zinafichua mabosi wa Man United kwa sasa wanafanyia kazi jambo hilo na wapo tayari kulipa ada ya Pauni 80 milioni ya awali na kisha italipa bonasi nyingine baadaye.

Hata hivyo, ripoti zinadai kuna wazo jingine linamhusisha Sancho kama sehemu ya ofa hiyo baada ya winga huyo kutokuwamo kwenye mipango ya Kocha Ruben Amorim huko Old Trafford.

Baleba anaripotiwa yupo tayari kwenda kukipiga Old Trafford, ambako mshahara wake utakwenda kuongezeka, huku akiongeza sura nyingine mpya baada ya timu hiyo kuwanasa Matheus Cunha, Bryan Mbeumo na Benjamin Sesko kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Sancho alitumikia msimu wa 2024-25 kwa mkopo Chelsea, alikofunga mabao matano na kuasisti 10 katika mechi 41 za michuano yote.

Chelsea ilikuwa na mpango wa kumbeba Sancho jumla, lakini imeshindwa kufikia makubalino na mchezaji huyo, huku suala la kushindwa kumbeba jumla mchezaji huyo kimewafanya wapigwe faini ya Pauni 5 milioni na Man United.

Sancho amekuwa akihusishwa sana na Juventus kwenye dirisha hili, huku ikibainishwa pia timu yake ya zamani Borussia Dortmund nayo kumsaka.