Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka, Odegaard ni presha tupu Arsenal

SAKA Pict

Muktasari:

  • Wachezaji hao wote walipata majeraha wakati timu yao ilipokipiga na Leeds United katika mchezo uliofanyika uwanjani Emirates, Jumamosi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA Mikel Arteta kijasho kinamtoka huko Arsenal baada ya mastaa wake Bukayo Saka na Martin Odegaard wote kuumia ikiwa bado wiki moja tu kabla ya kwenda kukabiliana na Liverpool kwenye mchakamchaka wa Ligi Kuu England.

Wachezaji hao wote walipata majeraha wakati timu yao ilipokipiga na Leeds United katika mchezo uliofanyika uwanjani Emirates, Jumamosi.

Nahodha Odegaard aliumia bega kwenye purukushani za kugombea mpira na mpinzani, akatolewa uwanjani na nafasi yake kuingizwa Ethan Nwaneri.

Arsenal ilikuwa mbele 1-0 wakati Odegaard wakati anaumia na muda mfupi baadaye, Saka alifunga bao baada ya nahodha wake Odegaard kutolewa.

Lakini, winga huyo matata kabisa wa Arsenal, Saka naye aliumia dakika nane baada ya kipindi cha pili kuanza. Na baada ya mechi, kocha Arteta alisema maumivu ya Saka yanamtia mashaka zaidi ya mwenzake Odegaard.

Alisema: “Majeruhi ndio kasoro ya siku hii. Martin alihisi maumivu kwenye bega lake aliloliangukia. Atafanyiwa vipimo kesho (jana).

“Bukayo alikuwa akikimbia na mpira na kupigana vikumbo na beki na kupata maumivu kwenye misuli. Kwa Bukayo kutoka nje, hicho ni kitu kinachotia shaka.

“Ngoja tuone. Ni maumivu mengi ya misuli na si yale ya kwanza. Tupo kwenye wiki ya pili ya msimu kuanza na tayari tumempoteza Kai, Martin na Bukayo. Hilo linaonyesha jinsi gani unapaswa kujiweka sawa kwenye ligi.”

Kwenye mechi hiyo ya Leeds, Arsenal ilishinda 5-0, huku straika wao Viktor Gyokeres akifunga mara mbili, ilimtangaza pia staa wao mpya, Eberechi Eze, iliyemnasa kwa Pauni 67.5 milioni kutoka Crystal Palace na kuwazidi ujanja mahasimu wao Tottenham Hotspur.

Kutokana na hilo, Arsenal ikikabiliwa na mechi ngumu ya kwenda kuwakabili Liverpool huko Anfield huku ikiamini Eze ataanza kuitumikia timu yake mpya.