Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saka atia tiki usajili wa Eze

Muktasari:

  • Arsenal inafikiria kutoa Pauni 70 milioni kunasa saini ya Eze, baada ya kumweka mkali huyo wa Crystal Palace kwenye orodha ya mawinga wapya inaowasaka baada ya kupata saini ya straika Viktor Gyokeres.

LONDON, ENGLAND: BUKAYO Saka amewasha moto baada ya kusikia mpango wa Arsenal wa kutaka kumleta Eberechi Eze kwenye kikosi hicho huku jambo hilo likidaiwa kuwapa raha kubwa mashabiki wa timu hiyo ya Emirates.

Arsenal inafikiria kutoa Pauni 70 milioni kunasa saini ya Eze, baada ya kumweka mkali huyo wa Crystal Palace kwenye orodha ya mawinga wapya inaowasaka baada ya kupata saini ya straika Viktor Gyokeres.

Eze, 27, ambaye ni shabiki wa Arsenal yupo tayari kujiunga na miamba hiyo ya Emirates na kinachoonekana ni kama vile Saka anakaribisha uhamisho huo utakaokwenda kuleta ushindani mkubwa wa namba kikosini.

Mwaka jana, Saka alimtaja Eze kuwa ni moja ya wachezaji wenzake kwenye kikosi cha England ambao wanamkosha sana mazoezini.

“Eze amekuwa na kiwango bora mazoezini,” alisema Saka, 23.

“Amekuwa akinivutia sana, naweza kusema hivyo.”

Saka si mchezaji pekee ambaye amekuwa akivutiwa na Eze mazoezini, baada ya beki Joel Lynch, ambaye alicheza na Eze huko QPR, aliwahi kusema alikuwa hamsogelei winga huyo kwenye mazoezi kwa sababu ya kuogopa kuumbuka.

“Nilikuwa simsogelei kabisa kwa sababu ni fundi sana na nilikuwa naogopa asinipige matobo,” alisema Lynch.

“Kabla ya mechi kuanza, nilikuwa namfuata na kugonga naye tano, kisha namwambia, hebu funga kwa ajili yetu zote, tusaidia kushinda tafadhali.”

Mabeki wa Arsenal watakuwa kwenye kasheshe zito la kumkaba Eze kwenye mazoezi yao ya kila siku endapo kama mkali huyo atajiunga na miamba hiyo kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.